ELIMU BURE TANZANIA ITAWEZEKANA?
Maoni yangu kuhusu waraka wa serikali juu ya
elimu bure.
Kwanza napongeza sana serikali kwa kusikiliza
kilio cha wananchi cha muda mrefu.
Pili swala la utoaji elimu linawadau muhimu
watano yaani.
1.Serikali
2.Waalimu
3.Wazazi
4.Wanafunzi
5.Jamii kwa ujumla.
Kama ilivyokawaida ya serikali yetu kufanya
mambo bila maandalizi wala tafiti ,hili la Elimu
bure tusipokuwa makini huenda likachangia
kudumaza kiwango cha Elimu nchini au
likaimarisha zaidi mfumo wetu wa Elimu.
Mpaka sasa baada ya tamko la serikali la kutoa
Elimu bure,wazazi wengi wanashangilia sana,
huku walimu ambao ni wadau muhimu wa sekta
ya Elimu wakiwa na mashaka sana juu ya tamko
hili.
Msingi wa mashaka ya waalimu unajengwa juu
ya mazoea yaliyojengwa na serikali yetu.
Pamoja na serikali kutangaza Elimu bure
waalimu wengi hawayaoni maandalizi yoyote ya
utoaji Elimu bure kama waraka wa serikali
unavyo elekeza.
Mimi nikiwa sehemu ya walimu pia ninatilia
shaka maandalizi ya serikali,
Shuleni yapo mahitaji madogo madogo mengi
yanayotakiwa kutumia fedha.
Mfano ni fedha kwaajili ya kuchapisha mitihani
ya majaribio ya kila wiki,Majaribio ya kila mwezi
na mitihani ya muhula wa kwanza na wapili.
Kabla ya tamko la serikali,waalimu walitumia
mbinu ya kuwachangisha wanafunzi fedha
kwaajili ya kuchapisha mitihani kwenye
stationary za watu binafsi.
Kwa maeneo mengi ya vijijini ambako shule
hazina umeme,kompyuta wala mwalimu anaejua
hata kuibonyeza hiyo key bord ya
compyuta,walimu waliwachangisha watoto kati
ya shilingi 2000/= na 3000/= ili kuchapisha
mitihani ya masomo tisa (9) atakayofanya
mtoto.
Walimu waliwashirikisha wazazi kuchangia
watoto wao ili kumpa fursa nzuri mwalimu
kutunga maswali mazuri, pia kumpa fursa mtoto
kujibu mtihani kwa upole tofauti na wakati
walimu wanaandika mtihani ubaoni,ambapo
mtoto alilazimishwa kujibu maswali kuendana na
speed ya mwalimu ili asifute ubao.
Sasa wakati wazazi wamejenga utamaduni wa
kuchangia eneo la mitihani,serikali imekuja na
tamko la kufuta michango yote shuleni,binafsi
kama nilivyoanza awali, naipongeza sana serikali
kwa usikivu wake lkn naomba sana kwa Mungu
tamko hilo lisitekelezwe kisiasa.
Napata mashaka makubwa kwasababu zifuatazo.
Kwanza mpaka leo tarehe 14-12-2015 hakuna
mwalimu mkuu wa shule yeyote wala Head
master aliyekwisha pewa maelekezo na Afisa
Elimu apeleke mchanganuo wa Matumizi ya
shule (bajeti) yake kwa kila mwezi,Muhula na
Mwaka.
Sasa shule zitafunguliwa wiki Mbili
zijazo,zinaenda kufunguliwa huku serikali ikiwa
haina mchanganuo wa matumizi ya kila shule ili
iweze kupeleka Fedha shuleni kulingana na
mahitaji.
Serikali isijidanganye kuweka kiwango sawa (flat
rate)cha matumizi kwa shule zote Tanzania.
Maana shule zinatofautiana mahitaji kutokana na
mazingira na idadi ya wanafunzi.
Wakati kuna shule ambazo walau zina miradi
kama minara ya simu,Flame za maduka nk ,zipo
shule ambazo hazina mradi wowote ule hasa
shule nyingi za vijijini ambazo ni zaidi ya 70% ya
shule zote Tanzania.
Kama mpaka leo hakuna tathmini yoyote ya
matumizi ya shule iliyoombwa na Afisa Elimu au
kiongozi mwingine wa Serikali ili kuanza
mchakato wa allocation ya fedha za kuendeshea
shule,huku wazazi wakiwa tayari wana uhakika
(guarantee) ya kutochangia jambo lolote,naona
Zigo hili likirudi kuwaangukia walimu.
Walimu watarudi kuandika tena maswali hamsini
ubaoni,walimu watachangishana sehemu ya
fedha za mshahara wao kuchimba choo
kilichobomoka kwa sababu ya mvua.
Matokeo yake tamko la serikali huenda likaondoa
zaidi morali ya walimu ya kufanya kazi kuliko
kuwajengea motisha
Hayo yakitokea basi litatokea anguko kubwa la
Elimu Tanzania(Mass Education failure)
Ikitokea serikali ikafanikiwa kuzifahamu bajeti za
shule kwa muda uliobaki tutakuwa tumepata
ushindi mkubwa katika ukuaji wa elimu
Tanzania,watoto ambao wazazi wao hawana
uwezo wa kuchangia watakuwa wamekuwa huru
na watasoma kwa amani.
Changamoto nyingine itakayoibuka endapo fedha
zitaanza kuletwa na serikali,basi ni
ucheleweshaji wa fedha kuwafikia walengwa.
Wapo viongozi wa serikali ambao kwao Elimu si
kipaumbele sana kama sekta zingine za serikali.
Viongozi kama hao hawatashindwa kutumia
fedha za Elimu kujengea daraja lililo katika kwa
madai kuwa fedha za daraja zikifika zitafidiwa
kwenye Elimu. Wenyewe wanaita kubadili
matumuzi (Reallocation)watahamisha hizo fedha
kwenda maeneo mengine .
Na wapo baadhi watathubutu kuzitumia hizo
fedha kufanyia biashara ili kutengeneza kwanza
faida kisha ndio zipelekwe shuleni.Yapo
malalamiko ya muda mrefu yanayodai kuwa
fedha za halmashauri zinapelekwa kuzungushwa
kwanza kisha ndio ziwafikie wakengwa,hawa
jamaa hata mshahara ya watumishi walikuwa
wanaanza kuzungusha kisha ndio watumushi
wanalipwa,
Amani ya watumishi imerejea hivi karibuni baada
ya mishahara kutokea Hazina moja kwa moja
bila kupitia mikononi mwao.
Hivyo nashauri serikali kama itafanikiwa
kupeleka Fedha shuleni,basi shule zipewe aidha
Check number maalum au Account namba
maalum ili kila shule iingiziwe fedha zake za
ruzuku moja kwa moja kutoka Hazina bila kupitia
mikononi mwa wajanja wajanja.
Hii itasaidia sana fedha kuzifikia shule kwa
wakati bila walimu wakuu na wakuu wa shule
kudaiwa 10% na waliowateua.
Maafisa Elimu wabaki na majukumu ya kiutawala
(adminstrative role)kwaajili ya kuhakikisha
walimu wanawajibika kutimiza wajibu wao bila
visingizio.
Wakati huo serikali itafute namna bora ya
kuboresha maslahi ya walimu ili kuwafanya
wasijisikie wanyonge .
Hayo yakifanyika Tanzania itakuwa kisima cha
maarifa na sekta ya elimu itachochea
maendekea makubwa kutokana na nchi kuwa na
rasilimali watu ya kutosha kuendesha sekta
zingine za serikali na za binafsi.
Mwl Jashia Khamisi Maarufu.
0765733718/0714276818
0 comments :
Post a Comment