-->

HIKI NDICHO KILICHOMFANYA DR. MAURICE BUCAILLE AWEZE KUSILIMU

DR. Maurice bucaille ambaye alikuwa mwana sayansi mashuhuri Sana, yeye ndie aliyechaguliwa kwa ajili ya kufanya uchunguzi katika mwili wa firauni (pharaoh), ili ijulikane sababu ya kifo chake,
Kabla ya kufanya uchunguzi alikuwa mkiristo, na katika biblia imeelezwa kuwa firauni (pharaoh) hakuzamishwa na na bahari Bali alikufa kifo cha kawaida, lakini Dr. Maurice bucaille alipochunguza mwili wa firauni (pharaoh) alipata mchanga wa bahari katika mwili wake. Ambapo ilikuwa ushahidi uliodhaahiri kuwa firauni (pharaoh) alizamishwa na bahari,
Wakati wa uchunguzi Kuna mtu alimuambia kuwa katika kitabu cha waislamu kiitwacho Quran imeandikwa habari kuhusiana na firauni (pharaoh), (AL Quran 10:90-92)
90.
Tukawavusha bahari Wana wa Israili, na Firauni na askari wake wakawafuatia kwa dhulma na uadui. Hata Firauni alipo kuwa anataka kuzama akasema: Naamini kuwa hapana mungu ila yule waliye muamini Wana wa Israili, na mimi ni miongoni mwa walio nyenyekea!
91.
Ala! Sasa? Na hali uliasi kabla yake na ukawa miongoni mwa mafisadi!
92.
Leo, basi, tutakuokoa kwa mwili wako, ili uwe Ishara kwa ajili ya walio nyuma yako. Na hakika watu wengi wameghafilika na Ishara zetu.
Al Qur’an 10:90-92
Baada ya kusikia habari hii alishangaa Sana, akasema Quran ilikuja Baada ya miaka 2000 kupita tangu kifo cha firauni (pharaoh). Na mwili wake uligunduliwa 1898, na hakuna aliyemjua firauni kwa miaka 35000 kimakadirio,
Lakini Quran kumbe ishaeleza habari zake, na pia Quran imeelezea ishara Za firauni (pharaoh), leo ishara zote zimekubaliwa katika uchunguzi,
Na Baada ya Hilo ALHAMDULILLAH yeye akatangaza kuwa ni muislamu na kutoa shahada
ALLAH HU AKBAR
TANGAZO LA NDANI===
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment