-->

PALE TAIFA STARS ILIPOINGIA UWANJANIVIFUA WAZI

Pichani ni aliyekuwa Rais wa Sudan, Bwana
Jaafar
Mohammed Numeir (Wa kwanza Kulia Mwenye
Suti)
akiongozwa na Nahodha wa Timu ya Taifa ya
Tanzania, Bwana Abdulrahman Juma (Katikati
Mwenye Kaptula Nyeupe) kusalimiana na
Mchezaji
wa Nguli wa Taifa Starz Bwana Omar Zimbwe
huku
Wachezaji wa Taifa Starz wakiwa Vifua wazi bila
Jezi .
Wa Kwanza Kushoto anayeangalia ni Mchezaji
Mohamed chuma "Shoto" na wanaonekana
nyuma
ya Nahodha Abdulrahman ni Wachezaji
Mashuhuri
Kitwana Manara "Popat" na Abdallah "King"
Kibaden
Mputa, hapa ilikuwa katika Uwanja wa Uhuru
(Uwanja wa Zamani wa Taifa, Jijini Dar es
salaam).
Watu wengi wanapenda kuandika kuwa Mechi hii
Taifa Stars walicheza vifua wazi (Bila Jezi) na
sudan baada ya kukosekana jezi, Lakini ukweli
wa
mambo haukuwa hivyo bali kilichotokea ni kuwa
Timu zote Mbili zilikuja Uwanjani zikiwa na Jezi
zinazofanana.
Kwa mujibu wa Kanuni, Sheria na Taratibu za
Shirikisho la Soka Duniani, FIFA ni kwamba
kunapotokea Timu mbili zina jezi zinazofanana
basi
ile ambayo iko nyumbani (Wenyeji) ndiyo
inatakiwa
ibadilishe jezi, Taifa Stars hawakwenda Uwanjani
na Jezi za Ziada.
Mara baada ya Ukaguzi uliofanywa na Rais
Jaafar
Mohammed Al- Numeir wa Sudan Starz
waliletewa
Jezi Nyengine na ndipo Mpira ukaanza huku Rais
wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,
Mwalimu
Julius Kambarage Nyerere akiwa Uwanjani hapo
kushuhudia Aibu hiyo ya Mwaka.
MECHI ILIKUWA NI DHIDI YA SUDAN NA
INASEMEKANA ILIKUWA NDIO MECHI YA
MWISHO MWALIMU KWENDA UWANJANI
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment