Mshambuliaji Mbwana Samatta atajiunga na klabu ya KRC Genk ya
Ubelgiji baada ya timu hiyo kukamilisha usajili wake kwa kitita cha Euro
2.5 milioni zinazokaribia Sh 6 bilioni.
Uhamisho huo wa Samatta umekuja baada ya mmiliki wa klabu yake ya TP Mazembe, Moise Katumbi kufikia makubaliano na Genk juu ya mauzo ya mchezaji huyo na tayari Samatta ameshasaini mkataba wa miaka minne na nusu wa kuichezea timu hiyo ya Ubelgiji.
Akizungumza na gazeti hili jana, wakala wa mchezaji huyo, Jamal Kisongo alithibitisha kuwa tayari Samatta ameshasaini mkataba na Genk na kwa sasa yupo nchini kwa ajili ya mapumziko baada ya kumaliza mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Dunia.
“Ni kweli Samatta ameshakamilisha uhamisho wake kutoka Mazembe kwenda Genk ambao kwa kiasi kikubwa ulisimamiwa na Rais wa Mazembe, Katumbi, ambaye alikutana na uongozi wa timu hiyo ya Ubelgiji kwa ajili ya majadiliano ya kumuuza Samatta,” alisema Kisongo.
Ingawa Kisongo hakutaka kuweka wazi kiasi cha pesa kilichotumika kwenye uhamisho wa Samatta, habari za uhakika ambazo gazeti hili limezinasa ni kuwa uhamisho wa Samatta utagharimu kiasi hicho cha fedha (Sh 6 bilioni).
Kwa mujibu wa Kisongo, Simba ambayo ilimuuza Samatta kwa TP Mazembe itanufaika na mauzo ya mshambuliaji huyo kutokana na uwepo wa kipengele kwenye mkataba wake kinachoonyesha kuwa timu hiyo inatakiwa kupata mgawo wa asilimia fulani ya pesa kwenye mauzo ya Samatta. Lakini hata hivyo, kituo kilichomkuza Samatta cha Jaki Academy hakitonufaika na mauzo ya mchezaji huyo ingawa kitanufaika na fedha ya kumkuza Samatta kwani bado hajavuka umri wa miaka 23 kama kanuni za Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) zinavyoainisha.
Genk inayoshiriki Ligi Kuu Ubelgiji, kwa sasa inashika nafasi ya sita kwenye msimamo na ni miongoni mwa timu zilizoibua mastaa kadhaa wanaotamba kwenye soka duniani kwa sasa kama Divock Origi anayechezea Liverpool ya Uingereza.
Wachezaji wengine waliopitia kwenye timu hiyo na timu wanazochezea sasa kwenye mabano ni kipa Thibaut Courtois (Chelsea), Kevin De Bruyne (Manchester City FC), Steven Defour (Anderlecht), Yannick Ferreira Carrasco (Atlético Madrid) na Christian Benteke (Liverpool).

0 comments :
Post a Comment