Je, umewahi kukamatwa na polisi wakati
ukiendesha gari, pikipiki au baiskeli?
zijue haki na wajibu wako !
Bila kufuata sheria na kanuni za usalama
barabarani kutakuwa na vurugu katika barabara
zetu.
Soma na ujifunze kanuni, Sheria Mpya za
Barabara – iwapo kila mmoja atazifuata sote
tutafika tunapokwenda kwa urahisi na usalama
zaidi. Polisi wana kazi ngumu na muhimu sana
ya kutekeleza sheria. Lazima kushirikiana nao,
isipokuwa kama wanatenda kinyume na sheria.
Maelezo hayo ni muhtasari wa mwongozo wa nini
ofisa wa polisi aliyevaa sare anaweza kufanya
kisheria na kukueleza ni wakati gani
anakusimamisha uwapo barabarani.
Mamlaka ya kusimamisha gari lako:
Ofisa wa polisi ana haki ya kusimamamisha gari
lako – kama atakupa ishara ya kusimama,
punguza mwendo kwa usalama na utoke
barabarani – pia anaweza kukuuliza jina na
anwani yako na ile ya mmiliki wa gari (Sheria ya
Usalama Barabarani (RTA),s.78).
Leseni ya kuendesha gari:
Ofisa wa polisi anaweza kuomba kuona leseni
yako yakuendesha gari – anaweza kukataa
fotokopi – hata hivyo, unaweza kuamua kupeleka
leseni yako ndani ya siku tatu kwenye kituo cha
polisi kilichochaguliwa na ofisa. Ili kuepuka
matatizo, wakati wote tembea na leseni yako
kwenye gari (RTA s.77).
Hati ya usajili:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua maelezo ya
usajili kama yanavyoonyeshwa kwenye kibandiko
cha usajili – gari lazima liendane na maelezo ya
kwenye kibandiko, lakini vitu vidogo kama rangi
iliyofifia au iliyobanduka haijalishi (RTA s.13).
Leseni ya barabarani, na bima ya gari:
Ofisa wa polisi ana haki ya kukagua kama
umebandika leseni halali ya barabarani na
kibandiko cha bima kwenye kiwambo cha upepo
cha gari lako (kioo cha mbele).
Kunyang’anywa:
Ofisa wa polisi HANA haki ya kuondoa vibandiko
na kuchukua leseni isipokuwa kwa mujibu wa
sheria.
Mikanda ya kiti ya usalama:
Wewe na abiria wako wa kiti cha mbele ni lazima
mfunge mikanda ya kiti ya usalama
unapoendesha (gari iwe inatembea au
imesimama) – unatenda kosa kama unaendesha
wakati abiria wako hajafunga mkanda wa kiti wa
usalama (RTAs.39.11). Hata hivyo inashauriwa
abiria wote wafunge mikanda.
Kuendesha baada ya kunywa pombe :
Kama ofisa wa polisi anakuhisi umekunywa
pombe na huwezi kulidhibiti gari
ipasavyo,anaweza kukutaka upimwe (kipimo cha
kupumua au kipimo cha damu) kuona kama kiasi
cha pombe kwenye damu yako ni zaidi ya
kiwango kilichoelezwa. Kama ukikataa utakuwa
na hatia ya kosa (RTA s.44, s.45, s.46).
Kutumia simu ya mkononi wakati unaendesha:
Ingawa sheria haikatazi hili mahususi, ofisa wa
polisi anaweza kuona kuwa unatenda kosa la
“kuendesha kwa uzembe” (RTA, s.42, s. 50).
Mwendo kasi:
Unapaswa kuzingatia kikomo cha mwendo kasi,
(ikiwa Ni pamoja na km 50kwa saa katika
maeneo ya hatari, ambayo yanaweza yasiwe na
alama) – ofisa wa polisi anaweza kupima
mwendo kasi wako kwa namna mbalimbali - hata
hivyo, unaweza kupinga ushahidi wake
mahakamani (RTA s.51, s.73 (2)).
Kustahili kuwepo barabarani :
Ofisa WA polisi ana haki ya kukagua Kama gari
lako liko katika hali ya usalama kiufundi. Matairi,
breki, taa, indiketa na usukani lazima viwe
vinafanya kazi vizuri –unawezakutakiwa kupeleka
gari mahali litakapokaguliwa kikamilifu na
mkaguzi wa magari wapolisi (RTA, s.39.1,
s.81).Unashauriwa kupeleka gari lako kukaguliwa
na polisi kila mwaka. Pata stika ya usalama
barabarani, cheti cha ubora wa gari, au barua
kutoka polisi kama ushahidi kwamba gari lako
limekaguliwa.
KAMA OFISA WA POLISI ANAKUTUHUMU
KWAMBA UMEFANYA KOSA : Mara nyingi
utapewa uchaguzi wa kukubali kosa na kulipa
faini ya sh. 20,000 kwa ofisa wa polisi, au
kwenda mahakaman ili kujibu mashtaka. Ofisa
ataandika maelezo kwenye Fomu ya Polisi ya PF
101, na nyote wawili mtatia saini – kamwe
usilipe faini bila ya kupata nakala ya Fomu
iliyotiwa saini. Unaweza kwenda Na ofisa kwenye
kituo cha Polisi kutoa maelezo. Kama unakubali
kosa, lakini huwezi kulipa faini, ofisa wa polisi
atakueleza jinsi ya kutuma malipo kwa kamanda
wake wa eneo (RTA, s.95).
KAMA UNAFIKIRI OFISA WA POLISI AMETENDA
KINYUME CHA SHERIA AU AMEKOSEA KWA
NJIA YOYOTE UNAWEZA KUTOA MALALAMIKO:
muulize ofisa jina lake, cheo na namba, na
anwani ya kituo cha polisi anakofanyia kazi
(unayo haki ya kuuliza hilo.) Kisha peleka
malalamiko ya maandishi kwa Ofisa Msimamizi
Mkuu – ambaye atachunguza na kujibu.
Tusaidie kuwafanya maofisa polisi wetu kuwa
waaminifu –usitoe rushwa na usipokee rushwa.
Unaweza ukapenda kukata maelezo haya na
kuyaweka kwenye gari lako – lakini kumbuka
kwamba ni mwongozo tu.

0 comments :
Post a Comment