-->

Dr Juma Mwaka amefanya kosa gani Na Sheria inasema nini ?



Tangu Naibu Waziri wa Afya afanye ziara iliyoitwa ya kushtukiza katika kituo cha Foreplan Clinic kinachoendeshwa na Tabibu wa Tiba Mbadala Dr Juma Mwaka na taarifa kuenea kuwa Dr Mwaka alikimbia na wauguzi wake nao kutoweka, kumekuwa na mjadala mpana kwenye mitandao ya kijamii watu wakikinzana juu ya nini hasa kilichotokea.
Wako watu waliopongeza hatua ya Naibu Waziri na wako wengine wanaohoji juu ya kilichotokea. Jamii imegawika.
Binafsi nimefuatilia mijadala kadhaa na mwishoe nimeona niulize swali Dr Mwaka amefanya kosa gani?
Baadhi wamedai kosa lake ni kujiita Dr Mwaka, wakijenga hoja kuwa Dr ni mtu mwenye leseni ya kutibu, kufanya upasuaji, au tabibu wa meno n.k pia anakuwa na shahada katika kada hiyo.
Nimeshangaa hoja hiyo. Kama kila Dr lazima awe tabibu (medical practitioner) mbona kuna watu wengi wanaitwa ma-Dr ambao sio matabibu?
Kwenye kada ya sheria;
Dr Harrison Mwakyembe, Dr Tulia Akson, Dr Masumbuko Lamwai, Dr Cuthbeth Tenga n.k hawa ni ma Dr wa sheria lakini sio matabibu.
Kwenye kada ya Dini;
Dr Getrude Lwakatare, Dr Wibroard Slaa, Dr Alex Malasusa, Dr Sulley n.k hawa ni ma Dr wa dini lakini sio matabibu.
Kwenye kada ya Taaluma;
Dr Benson Bana, Dr Azaveli Lwaitama, Dr Abdallah Posi n.k hawa ni ma Dr lakini sio matabibu.
Kwenye kipengele cha Heshima;
Dr Reginald Mengi, Dr Jakaya Kikwete n.k hawa ni ma Dr wa Heshima (Honorary Doctorate) lakini sio matabibu.
Kwenye michezo ya kuigiza;
Dr Cheni sio tabibu.
Kwenye Tiba Mbadala;
Dr Matunge, Dr Rahabu Rubago, Dr Isaac Ndodi, Dr Sigwa, Dr Samson Kibona, Dr Manyaunyau, Dr Mwaka n.k hawa ni ma Dr wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala
Kosa la Dr Mwaka ni lipi?
Wako wanaosema kosa lake ni kujitangaza. Mbona ana vibali rasmi kujitangaza?
Nyaraka zake zinaonesha ameruhusiwa kufanya anachofanya.
SHIRIKA LA AFYA DUNIANI WHO LINASEMAJE KUHUSU SERA ZAKE KUFIKIA MWAKA 2039 KUHUSU TIBA ASILI NA TIBA MBADALA?
Moja ya sera ya shirika la afya duniani ni kuleta mahusiano makubwa katika tiba kati ya tiba asili na tiba ya kisasa yani modern medicine. Na hiki ndicho kilichofanyika China,india na mataifa mengine yaliyo endelea.
Unapokuwa china kuanzia ngazi ya dispensary kuna kitengo cha tiba asili na tiba mbdala hadi ngazi ya rufaa. Kwa kutekeleza hilo agiza Tanzania imeanza kwa kutengeneza TANZANIA INSTITUTE OF HERBAL MEDICINE ambayo inaendeshwa chini ya wizara ya afya na ustawi wa jamii katika chuo kikuu cha Muhimbili hadi sasa kuna Masters za herbal medicine. Sasa tunatakiwa kujua taifa au ulimwengu unaenda wapi, Tunahama kwenye kutibu kienyeji kwa ramli,matunguli, na unga ambao hauna kiwango tunasafiri kutoka kwenye LOCAL TRADITIONAL MEDICINE TUNAENDA KWENYE MODERN TRADITIONAL MEDICINES. Nchi kama china hadi sasa dawa za TRADITIONAL CHINESE MEDICINES ndio ngumzo katika soko zinazodhoofisha soko la viwanda vingi vinavyo tengeneza dawa za kemikali.
Kutokana na sera na mbio za mabadiriko hayo, na sera moja wapo ni kuacha kuhangaika kutibu dalili za magonjwa na kuanza kutibu chanzo kuanzia kwenye seli na viini lishe ndani ya seli. Hivyo ndio vifaa vya uchunguzi km vyakutumia compyuter ambavyo wenzetu kule hata family physician [Dakatri wa nyumba kumi ulaya] wanatumia kuangalia homoni zako,micronutrients,macronutrients nk. Sasa kwa nini Dr mwaka akitumia mnashangaa? Kuna mashine siku hizi ambazo zinatumika katika kutibu magonjwa mbalimbali, km msongo wa mawazo,maumivu ya misuli,kukosa usingizi, nk kupitia Thermal therapy, huwa nakutana na madakatri wenzangu wanavipinga! Huwa nacheka sana unapinga kitu ambacho kimefanyiwa dafiti na mtu mwenye elimu kukuzidi na kimeruhusiwa kutumia kidunia, wewe unapinga kwa kutumia mgongo wa udakatri na sio nyalaka na tafiti za kisomi kama kweli wewe ni dakatri na umefuzu vizuri ‪#‎FANYA‬ TAFITI KUHUSU VIPIMO NA TIBA HIZO UTULETEE DATA ZAKE ! Hapo ndipo utamgundua msomi na mvivu,mwenye chuki na asiyependa maendeleo ya wengine kila siku majungu. HEBU TUWEKE ELIMU PEMBENI KILA MTU AFANYE KAZI YAKE KATIKA NAFASI YAKE.
Moja ya sera ya kusajili madakatri wa Tiba asili wote ilikuwa na kuwatambua wote na kile kibali kinaonesha kabisa kama una Meno au ngozi au kitu chochote cha mnyama hakikisha unakisajili. Na hicho kibali kinazuia kubaini magonjwa kwa njia ya RAMLI.
Sasa Swali Mlitaka Dr mwaka apige Ramli ndipo ajue kuna Fibroids au Ovarian Cysts au PID?
Ndio maana taifa linaenda kwenye MODERN TRADITIONAL MEDICINES, Na endapo wataalamu wa afya msipo kubaliana na hili mtaaanguka kabisa na mtapotea kama vyama vya siasa vinavyopotea.
Hivi Mwaka anashindwa nini kusaidiana na wasomi wa Picha za mionzi Radiologists na hatimaye mwaka kupata jibu sahihi amtibu vipi mgonjwa? Tatizo Wataalamu wa afya wengi maisha ni magumu, na Walifikiria kusoma udaktari basi maisha yamenyooka, bado ni omba omba na hadi sasa hawezi hata kulipia kipindi cha ITV Unazani atakula nini kama vipindi kwa mwezi ni zaidi ya milion 3? Mshahara wake hapo Anakusanya miezi 2.
Kwa nini TUWE NA USHABIKI USIOKUWA NA MAANA YOYOTE?
Tatizo siwezi kuwa laumu sana baadhi ya watalaamu wa afya maana Mitaala yetu inatunyima uwanja wa kufikiri sana kwa sababu hizi;
-Unasoma shule kwa kutumia Mtaala wa chuo kikuu wa kuchukua Doctor of medicine.
-Unamaliza unawaza kuajiliwa tu, huwazi hata kutumia elimu yako kufanya tafiti nyingi kututatulia hizi sintofahamu sio kukaa unahangaika kutype kitu ambacho kinakurudisha nyuma kimaendeleo kwa kumwengea mtu ambaye amekuzidi chochote ulicho nacho hapo ulipo. FANYENI TAFITI WASOMI MANENO HATUTAKI KABISA MSOMI ONGEA KWA TAFITI SIO KUTUMIA UBAVU WA ELIMU YA MIAKA 7 AU KUMI.
-Ukimaliza chuo unatukiwa Doctor of Medicine degree unakutana na Guidelines yani hizi ni miongozo ya matibabu ya kimataifa na taifa.
Kuna Tanzania Treatment Guidelines na WHO Treatment guidelines. Hii miongozi inatufanya tuwe watu wakukalili tu bila kuwaza vitu vikubwa, Our mind is locked in the guideline. Yani yeye akisha kalili guideline ya kutibu malaria basi ameshakuwa Dr. Milele na milele.
Sasa Hebu akili zetu tuzitumikishe kabisa maana najua Future ya Dr mwaka ni kubwa sana kwa sababu hata hiki cheti mnachokiona ni mwaka mmoja kinaweza kuwa ni thamani kubwa kuzidi matarajio yenu.
Siku moja nilikuwa najaribu kuchambua kwa nini CHINESE TRADITIONAL MEDICINES NI MOST RANKED MEDICINES IN THE WORLD AND FIRST CLASS HERBAL MEDICINES? Kile kitabu kimenifumbua mengi na nimeshangazwa na kazi kubwa Dr mwaka aliyo ifanya kusomea mimea ya nchini china na tafiti za mimea ya china jinsi gani zinatibu magonjwa tabia.
"Tiba ya kisasa ina nafasi yake katika kutibu magonjwa, lakini pia tiba ya asili ina nafasi yake kubwa mno"
TATIZO TANZANIA TUNAPUNGUKIWA NA TAFITI KUHUSU TIBA ASILI NA WASOMI WENGI WANAIBEZA NA KUISHUSHA HADHI BILA KUJUA KUWA DAWA NYINGI ZINATOKA HUKO.
Watu wanasema Dr mwaka anawachunguza watu sehemu za siri! Huku hana elimu ya kumchunguza mgonjwa!
Hata Dakatri hatusomei kumchunguza mgonjwa sehemu za siri. Na ndio maana daktari hata kama wewe ni profesa ukamchunguza mgonjwa sehemu za siri bila ridhaa yake utakuwa umekiuka misingi ya udaktari. Sasa kuchunguzwa huko ni ridhaa kati ya Dakatri na mgonjwa usikubali kwa kinyongo kisa yeye ni dakatri hapana kama una nafsi ya kukataa kataa kabisa.
Sasa Hivi hawa wanaochunguzwa hawakutoa lidhaa? Kama hawakutoa ridhaa mbona hawakwenda kushitaki? Yani mimi nashindwa kuelewa watu tunawazia wapi.
Unakutana na mtu anasema Wanawapotezea wagonjwa Muda wanakuja Wamezidiwa.
Hivi mara ngapi mgonjwa wa kisukari,presha,uvimbe anahudhuria hospital bila mafanikio? Tena kila akija Dawa zinaongezwa na pesa juu ya kumwona daktari bingwa wa magonjwa hayo. Je mtu kwenda kwa Mwaka kujaribu kupata matibabu yake kuna kosa gani km huku ameshindwa kupona? Kwani afya ni Ridhaa ya Dakatri au yangu? Mimi ndio mwenye ridhaa ya afya yangu!
Mara ngapi unaposema wagonjwa hawaponi wanawaibia pesa, Hivi mara ngapi wagonjwa hawaponi hadi wengine hospitali wanachukua dama! Kwani mbona kila hospitali ina chumba cha maiti? Kwani Dr Mwaka Mungu kila mtu apone jamani? Duuu, huwa nasema modern medicines Dr wangekuwa kwenye taifa la waelewa wangeishia pabaya, maana wanataka wao wanachokifikiria tu ndio kiwe chema cha mwingine kiwe kibaya.
TIBA ASILI NA TIBA MBADALA UKILINGANISHA NA TIBA YA KIZUNGU NI PAKA NA PANYA.
Unaposema Mwaka ni Biashara tu, basi sema Dawa hizo za hospitali ziwe bure kabisa na kusiwepo na pesa ya kumwona daktari tuone kma kuna baadhi ya watumishi wa afya wataishi hapa duniani.
Wengine wanasema Gharama kubwa za matibabu kwa Dr mwaka anawaibia.
Nakupa Zoezi dogo tu kama msomi na mwelevu, Eating Organic is Expensive, Jaribu kula vyakula vya asili, matunda km blue berries, strawberries,cranberries,bittermelon,watermelon nk ,mboga za majani kma broccoli,caulifolwer, Celery nk utaona gharama kwa mwezi shilingi ngapi! Tuone kama utamudu na kamshahara hako, ndio maana watu wanaishia kula Chapati, wali,viazi,juisi ya 1000 soda ya 500 na kuishia kupata magonjwa ambayo yanawagarimu maisha.
Unaposema ni gharama jiulize swali ukiambiwa kula vyakula asili utaweza gharama?
Basi ndio maana ni gharama maana mengine matunda na mbegu zake upataiakanji ni shida sana.
SIO MUDA WAKUIBEZA TENA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA, KINACHOTAKIWA NI KILA MTU AFANYE KAZI KATIKA NAFASI YAKE NA KUTIMIZA MAJUKUMU.
TIBA YA KISASA NA TIBA MBADALA ZOTE ZIPO KIBIASHARA MAANA HAKUNA HUDUMA INAYOTOLEWA BURE KATIKA KILA IDARA HIZO MBILI.
Utofauti mkubwa katika tiba asili na tiba ya kisasa ni DAWA ZINAZOTUMIKA KUTIBIA MGONJWA.
Mfano: Daktari wa kisasa amebobea kutibu kwa dawa za kisasa ambazo zinamtaka Anayetumia kitiba awe amesomea na anaujua mwili wa binadamu vizuri.
Daktari wa tiba asili, yeye amebobea katika mimea yake na anaujuzi wa kina kujua hii dawa yangu ninapo mpatia mgonjwa inaenda kutibu kitu gani na inafanyaje kazi mwilini? Ndio maana watu wanagundua dawa za asili, kama ginsen herb tablets,Gingko biloba tablets, Cordceps sinensis capsules hizo ni baadhi ya dawa asili zinazokamata headlines hata ktk ulimwengu soma medscape na Rejea zingine sio kusoma vitabu vya mitaala tu mnakuja kutoa maneno ya wivu yanaonesha kabisa maneno ya mshindwaji.
Sasa unapokuja kusema Daktari wa tiba asili asichambue mwili wa binadamu kama aliusomea ina maanisha huna imani na dawa zake! Maana atatumiaje dawa ambazo yeye hajui zinafanya kazi kivipi ktk mwili wa binadamu? Inasikitisha tunashindwa kuwaza haya.
Tafiti za tiba asili zipo na zinaendelea na kama Dr mwaka ni Tabibu anaruhusiwa kuendesha tafiti za kisayansi na akagundua dawa.
Tunacho angalia ni uwezo wa kuwafikia watu wengi na kuwasaidia wengi.
Kosa la Dr Mwaka ni lipi? Ambalo linamuhusu yeye peke yake na haliwahusu wenzake wa Tiba mbadala?
Boaz mkumbo.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment