Watafiti watatangaza matokeo ya uchunguzi kuhusu matumizi ya
dawa aina ya solanezumab, ambayo wagonjwa na wanasayansi wanatuami inaweza kuwa
tiba ya kwanza ya kupunguza kasi ya kupungua kwa kazi ya ubongo Dawa iliyopo
kwa sasa inasaidi kupunguza dalili , lakini haisitishi kufa kwa seli za ubongo.
Dr Eric Karran, kutokakituo cha utafiti wa maradhi hayo
nchini Uingereza , anasema dawa hiyo inaweza kuhakikishwa kuwa na "uwezo
mkubwa".
Maelezo ya uchunguzi kuhusu dawa ya solanezumab yatatolewa
katika mkutano miji Washington.
Dawa hiyo imekua matumaini makubwa ya malengo ya utafiti
unaolenga seli za protini ziitwazo amyloid ambazo humea kwenye ubongo mtu
anapokuwa na maradhi ya Alzheimer .
Inadhaniwa kuwa kuundwa kwa lundo la amyloid baina ya neva
za seli kunasababisha kuharibik na baadae kufa kwa seli za ubongo.
Majaribio ya sawa ya maradhi hayo yanayowakumba mamilioni ya
watu duniani yaligonga mwamba mwaka 2012.
Hata hivyo, wakati kampuni ya Marekani ya Eli Lilly
ilipoangalia kwa makini data, ilibainika kuwa kuna ishara inaweza kufanya kazi
kwa wagonjwa wanaoanza kupata ugonjwa huo.
0 comments :
Post a Comment