Yanga
wameshindwa kutamba kwenye uwanja wa nyumbani baada ya kubanjuliwa na
vigogo vya Kenya timu ya Gor Mahia kwenye mchezo wa ufunguzi wa michuano
ya Kagame Cup uliopigwa leo jioni kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Yanga
walitangulia kupata goli dakika ya nne kipindi cha kwanza kupitia kwa
mshambuliaji wao mpya Donald Ngoma walie msajili kutoka klabu ya FC
Platinum ya Zimbabwe lakini bao hilo halikuweza kudumu kwani Haruna
Shakava aliisawazishia Gor Mahia goli hilo dakika ya 16 ya kipindi cha
kwanza na timu hizo kwenda mapumziko zikiwa sare ya kufungana goli 1-1.
Mshambuliaji
wa Yanga Donald Ngoma alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha
kwanza baada ya kumpiga kwa makusudi mchezaji wa Gor Mahia.
Michael
Olunga aliifungia Gor Mahia goli la pili dakika ya 45 katika kipindi
cha pili na kuipa ushindi timu yake dhidi ya Yanga, mabingwa wa Tanzania
bara (Yanga) walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha lakini mambo
yalikuwa magumu kwa upande wao.
Nadir
Haroub ‘Cannavaro’ alikosa mkwaju wa penati baada ya mlinzi wa Gor
Mahia kuunawa mpira kwenye eneo la hatari wakati akiwa kwenye harakati
za kuokoa shambulizi lililofanywa na Yanga wakati wakilisakama lango la
Gor Mahia wakitafuta goli la kusawazisha.
Mabadiliko
yaliyofanywa na kocha wa Yanga Hans van der Pluijm kwa kuwaingiza
wachezaji Kpah Sherman akichukua nafasi ya Simon Msuva, Deusi Kaseke
akampisha Salumu Telela wakati Joseph Zutah akaingia kumpokea Juma Abdul
lakini mabadiliko hayo hayakuzaa matunda.
0 comments :
Post a Comment