-->

HAWA NDIO WACHEZAJI WANAOGOMBEA TUZO YA UCHEZAJI BORA

Messi vs PirloUEFA imetoa orodha ya wachezaji ambao wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Ulaya kwa mwaka 2015. Majina ya wachezaji waliocheza fainali ya UEFA Champions League kati ya Barcelona dhidi ya Juventus yametawala kwenye orodha hiyo huku Lionel Messi na Paul Pogba wakipewa nafasi ya juu kutwaa tuzo hiyo.
Winga wa Chelsea Eden Hazard pia ameingia kwenye orodha hiyo akiwa ni mchezaji pekee kutoka kwenye ligi ya England ambaye anapambana na wakali wengine kutoka La Liga na Serie A. Tovuti rasmi ya UEFA imetoa taarifa zaidi juu ya listi hiyo inayomjumuisha pia mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.
Ladha ya Barca-Juve imekuja bila kipingamizi. Miamba ya Catalan iliyoshinda vikombe vitatu msimu uliopita kwa kusaidiwa na washambuliaji watatu waliopewa jina la ‘utatu mtakatiu’  unaoundwa na Messi, Luis Suarez pamoja na Neymar ambao wote wapo kwenye orodha hiyo.
UEFA 2015
Wakati Juve wakitumaini kutwaa taji lao la tatu msimu huu waliangukia pua mbele ya Barca lakini bado Andrea Pirlo na Arturo Vidal wanaungana na Pogma kwenye orodha hiyo.
Wachezaji ambao walidhaniwa wangeinia kwenye orodha hiyo lakini wamepigwa chini ni pamoja na mshambuliaji wa Sevilla Carlos Bacca na winga wa Arsenal Alexis Sanchez. Bacca aliifungia Sevilla magoli 28 pamoja na kuisaidia timu hiyo kushinda taji la Europa League.
Wakati Sanchez yeye alifunga magoli 25 na kuisaidia Arsenal kutwaa taji la FA lakini kuenguliwa kwao kwenye orodha hiyo kumezua maswali mengi.
Watu wameanza kutabiri kuwa, mshindi wa tuzo hiyo atakuwa ni miongoni mwa wachezaji waliocheza fainali ya Champions League msimu uliopita huku Messi akipewa nafasi kubwa pamoja washambuliaji wenzie kutoka Barcelona.
Agosti 12 watatangazwa wachezaji walioingia tatu bora wakari msindi atatangazwa Agosti 28 Monaco, Ufaransa.
Share on Google Plus

About Unknown

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment