Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amefanya mabadiliko ya Utendaji katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kwa kumteua Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa
Uchaguzi.
Aliyekuwa Mkurugenzi Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC, Julius Mallaba.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amefanya mabadiliko ya Utendaji katika Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC) kwa kumteua Ndugu Kailima Ramadhani Kombwey kuwa Mkurugenzi wa
Uchaguzi.
Aidha, Rais Kikwete amemteua Jaji Richard Mziray kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vile vile, Rais Kikwete amewateua majaji wapya 13 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Vile vile, Rais Kikwete amewateua majaji wapya 13 wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Taarifa iliyotolewa leo, Jumamosi, Julai 25, 2015 na Ofisi ya Katibu
Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue mjini Dar es Salaam inasema kuwa
teuzi hizo zote zimeanza leo hii.
Kwa mujibu wa taarifa ya Balozi Sefue, Ndugu Kombwey ambaye anaapishwa
baadaye leo jioni, anachukua nafasi ya aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi,
Ndugu Julius Benedicto Mallaba.
Badala yake, Rais Kikwete amemteua Bwana Mallaba kuwa Jaji wa Mahakama
Kuu ya Tanzania. Kabla ya uteuzi wake, Bwana Kombwey alikuwa Mkurugenzi
wa Utawala, Tume ya Uchaguzi.
Taarifa hiyo pia imesema kuwa Jaji Mziray ambaye anateuliwa kuwa Jaji wa
Mahakama ya Rufani ya Tanzania kwa sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu, Dar es
Salaam.
Majaji wa Mahakama Kuu ambao wameteuliwa na Rais Kikwete, kwa mujibu wa
taarifa hiyo, Ndugu Ignas Pius Kitusi ambaye ni Msajili Mkuu, Mahakama
ya Tanzania, Ndugu Wilfred Peter Dyansobera ambaye ni Naibu Msajili,
Mahakama Kuu; Ndugu Lameck Michael Mlacha ambaye ni Naibu Msajili na
Mwenyekiti wa Baraza la Rufani la Kodi; Ndugu Salima Mussa Chikoyo
ambaye ni Naibu Msajili, Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi; Ndugu Isaya
Arufani ambaye ni Naibu Msajili na Katibu wa Jaji Mkuu wa Tanzania na
Ndugu Julius Benedicto Mallaba.
Wengine ni Ndugu Adam Juma Mambi ambaye ni Katibu Msaidizi, Tume ya
Kurekebisha Sheria; Ndugu Sirilius Betran Matupa ambaye kwa sasa ni
Msaidizi wa Rais, Sheria, Ofisi ya Rais, Ikulu; Ndugu Issa Maige ambaye
ni wakili wa kujitegemea, Ndugu Licia Gamunya Kairo ambaye ni wakili wa
kujitegemea; Dkt. Masoud Shaaban Benhaji wakili wa kujitegemea na
Mhadhiri Mwadamizi, Chuo Kikuu Huria, Dar es Salaam, Ndugu Victoria
Makani ambaye ni wakili wa kujitegemea na Ndugu Rehema Joseph Kerefu
ambaye ni mwanasheria wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Taarifa hiyo imesema kuwa wakati Ndugu Kombwey anaapishwa leo, majaji wataapishwa katika tarehe itakayotangazwa baadaye.
0 comments :
Post a Comment