-->

EDWARD NGOYAI LOWASA NA SIASA ZA TANZANIA

SIASA SIO MCHEZO!!!!!
Mwaka 1995 Mhe Edward Lowassa aliamua kuingia katika mchakato wa kumpata mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Wakati huo Lowassa aliombwa na Umoja wa Vijana kupitia kikao cha Baraza kuu la Taifa achukue fomu akiwa miongoni mwa wana CCM wanne ambao vijana waliamini wangeweza kulisaidia Taifa kupiga hatua za haraka kuelekea kwenye maendeleo endelevu, wengine waliokuwa waliokuwa wametajwa na Umoja wa vijana ni pamoja na Dkt Salim Ahmed Salim, Dkt Laurance Gama na Jaji mstaafu Mark Bomani.
Katika hatua ya kuchagua majina matatu kati y majina 11 yaliyoomba nafasi hiyo Mhe Lowassa akawa hakupendekezwa, lakini hakununa wala kususa bali aliamini kuwa Mwanamapinduzi mwenzie Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ataweza kutekeleza dhamira aliyokuwa nayo ya kuwaletea watanzania maendeleo, hivyo alirudi kwa makundi mbalimbali wakiwemo vijana wa CCM ambao walihoji kwanini ameenguliwa na yeye kwa utii mkubwa kwa CCM aliwataka vijana na viongozi wengine waheshimu maamuzi ya chama na kumuunga mkono Dkt Jakaya M Kikwete.
Ikumbukwe kuwa mwana-CCM mwingine aliyekuwa nakubalika kwa umma, Augustine Lyatonga Mrema aliamua kuondoka mapema CCM kwa sababu ndogo tu ya kubadilishwa wizara na kuamua kwenda chama cha NCCR Mageuzi ambako aligombea uraisi kwa chama hicho na kuleta upinzani mkubwa.
Yapo maneno ya baadhi ya wanasiasa kwamba kutoteuliwa kuwa Mgombea kwa Mhe Lowassa kulitokana na kuonekana anamiliki fedha nyingi akiwa na muda mfupi kwenye utumishi wa umma, lakini pia inasemekana kuwa wale watu waliohoji kukatwa kwa jina lake kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya Taifa, Walijibiwa kuwa, CCM iliamua kupeleka majina matatu kwenye mkutano mkuu ili wachague jina moja.
Katika uwakilishi huo wa majina walipenda apatikane mtu mzima mmoja, mwenye umri wa kati mmoja na kijana mmoja, ambapo watu hao ni
Mzee Cleopa David Msuya ambae ni mtu mzima,
Ndugu Benjamini Mkapa ambae umri wake ulikuwa wa kati na kijana ambae ni Jakaya Mrisho Kikwete.
Lakini maneno hayo ya baadhi ya wanasiasa hayakuishia hapo, wakadai kuwa baada ya Rais Mkapa kuchaguliwa hakumteua Mhe Lowassa kwa kuwa aliagizwa na Mwalimu Nyerere asimteue mpaka achunguzwe kama uwezo wa kiasi cha fedha alionao unatokana na mapato halali, na kama sio halali asimteue.
Mwaka 1997 Mhe Rais Benjamin Mkapa akamteua Mhe Lowassa kuwa Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa Rais - mazingira.
Kama maneno hayo ya baadhi ya wanasiasa ni ya ukweli basi uchunguzi ulifanyika na kuonekana mapato yake ni halali au vinginevyo unaweza kusema zilikuwa ni hisia tu za kimazingira.
Chanzo:- Wikipedia- Edward Lowassa.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment