Ramadhani Gembe mwanafunzi wa Feza boys aliyeongoza kitaifa matokeo ya kidato cha sita.
- “Nilitegemea ningefaulu lakini siyo kwa kiwango hicho… hii ni
‘surprise’ (shtukizo),” alisema Gembe alipohojiwa na Mwananchi baada ya
matokeo ya kidato cha sita kutangazwa na Baraza la Mitihani la Taifa.
- “Nawashukuru wazazi, walimu, ndugu na wanafunzi wenzangu kwa kunipa
ushirikiano.Nilikuwa nafanya sana ibada hivyo haya matokeo ni juhudi
binafsi na majibu ya Mungu,” alisema Ramadhani aliyesoma mchepuo wa
fizikia, kemia na baiolojia (PCB).
Historia ya Ramadhani darasani si haba kwani mwaka 2008 alikuwa ni
mwanafunzi pekee aliyejiunga na shule ya vipaji maalumu ya Ilboru,
Arusha akitokea shule ya Msingi Mombo na alipata daraja la kwanza akiwa
na pointi 11 katika matokeo ya kidato cha nne.
- “Siku zote kilichonifanya niongeze juhudi katika masomo yangu ni
malengo ya baadaye... mimi nataka kuwa daktari wa binadamu hivyo
sikutaka kulegalega kusoma.Pia, wazazi wangu pamoja na hali ngumu
walijitahidi kunisaidia kimawazo, kirasilimali na kimaadili…naomba na
wazazi wengine wawafanyie hivyo watoto wao,” alisema.
Baba Nurdin Gembe, ambaye ni mzazi wa Ramadhani, alisema familia
imepokea kwa furaha matokeo hayo na kwamba alikuwa akiyategemea kuwa
mazuri kutokana historia ya kijana wake katika madarasa ya nyuma.“Huyu
mtoto namlea kawaida japo zamani alikuwa mtundu sana… ilibidi nimpe
mafundisho mengi sana ya kidini bila kupoteza ratiba ya kusoma
shuleni.Nashukuru kuwa alizingatia na amefika hapo alipofika,”alieleza
Gembe ambaye ni bwana shamba kitaaluma.
0 comments :
Post a Comment