MakongoroKada wa Chama Cha Mapinduzi na mbunge wa Afrika Mashariki, Charles Makongoro Nyerere ametangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Kawe ikiwa ni siku chache baada ya kuridhia matokeo ya kutoteuliwa na chama chake kuwania kiti cha urais.
Makongoro ambaye ni mtoto wa hayati Mwalimu Julius Nyerere anataka kuwawakilisha wananchi wa jimbo hilo la Kawe ambalo hivi sasa linashikiliwa na Halima Mdee wa Chadema.
Hata hivyo, Makongoro anasubiri chujio la kwanza la kura za maoni la chama chake ili kumuwezesha kuwania kiti hicho cha Ubunge. Tayari makada wengine 14 wa Chama hicho wametangaza nia ya kugombea ubunge wa jimbo hilo wakiwemo Yusuph Nassoro, Mititi Butiku, John Mayanja , Dickson Muze na Dkt. Wilson Babyebonela.