Tovuti rasmi ya Simba imeripoti
kwamba Simba Sports Club kwa kushirikiana na Kampuni ya Tigo Tanzania
zimezindua huduma ya ujumbe mfupi ijulikanayo kama ‘SIMBA NEWS’, ambayo
lengo lake nikuwapatia wateja wa Tigo taarifa zinazoihusu klabu ya Simba
popote walipo nchini.
Huduma hii mpya inajulikana
kama ‘SIMBA NEWS’. Njia hii ni rahisi na yenye ufanisi yenye kuifanya
dunia ijulikane kwa wateja wake. “Pamoja na kasi yaukuaji wa Tehama,
Tigo inaelewa umuhimu wakutoa taarifa kwa wateja wake, ndiyo maana leo,
tunajisikia fahari kuzindua huduma hii iliyotengenezwa vizuri ya SIMBA
NEWS nawashirika wetu wa klabu ya SIMBA, EAG Group LTD pamoja na Premier
Mobile Solutions (PMS), ilikuendelea kuwapa wateja wetu taarifa
zinazohusu masuala ya sasa huku wakifurahia habari mpya zinazohusu
klabu,”alisema meneja wa mawasiliano ya kibiashara Jacqueline Nnunduma.
Lengo letu si tu kuwapatia
wateja wetu taarifa kiurahisi zaidi, lakini pia kuwapatia taarifa hizo
kwa wakati na zenye uhakika kutoka vyanzo vya michezo vyenye kuaminika,”
aliongeza Nnunduma.
Akizungumza kwa niaba ya Klabu
ya Simba,Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva alisema, “Tunaamini ubunifu
huu bila shaka utawawezesha mashabiki wote wa Simba na wa soka kwa
ujumla ambao pia ni wateja wa Tigo kupata habari mbalimbali za klabu ya
Simba kupitia simu zao za mkononi”.
Tunawahimiza mashabiki wetu
kujiunga na huduma hii kupitia Tigo ili waweze kupata nakufurahia habari
mbalimbali kutoka klabu ya Simba. Aliendelea Aveva.
Akiongea katika tukio hilo
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya EAG Group LTD Imani Kajula ambao ni
washauri na watekelezaji wa shughuli za kibiashara na masoko katika
klabu ya Simba, alisema “Tunatarajia kuendelea kuwapatia mashabiki wa
Simba huduma za kisasa kwa kutumia teknolojia zisizokuwa na usumbufu wa
aina yeyote kupitia wadau wanaoaminika ndani ya Tanzania”
Kwa upande wake Meneja
Uendeshaji wa Premier Mobile Solutions, Bi Lulu Ramole alisema kuwa
huduma hii imetengenezwa ili kuwawezesha wateja kupata habari za papo
kwa papo naaliongeza kuwa huduma ipo katika mfumo wa vifurushi vya Combo
/ BUNDLE PACK ambapo wateja wa Tigo watakuwa wakilipia mara moja kwa
siku na kupokea kiwango cha chini cha habari nne (04) na habari mpya za
kila siku zina zohusu klabu ya Simba.
Huduma pia itamruhusu mteja
aliyejiunga kujitoa kwenye huduma hii wakati wowote akitaka bila vikwazo
vyovyote na pia kwenye huduma hii kutakuwepo na neon kuu “MSAADA”kwa
ajili ya kusaidia juu ya maswali mbalimbali ya nayo ulizwa mara kwa mara
na wateja wakati wakifurahia huduma.
Ili kujiunga na huduma hizi
unatakiwa kutuma neon kuu SIMBA kwenda 15460. Utakapo jiunga tu mteja
atapokea habari kutokana na neon analolituma kila siku na atatozwa kiasi
cha shilingi za kitanzania 150 kwa siku. Na ili kujitoa kwenye huduma
mteja atahitaji kutuma neno ONDOA SIMBA kwenda 15,460
0 comments :
Post a Comment