-->

JESHI LA POLISI MBEYA LAWAITA KWENYE USALILI MBEYA VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE

AHMED Z. MSANGI – SACP-KAMANDA WA POLISI MKOANI MBEYA

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI


JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWAITA KWENYE USAILI VIJANA WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE MWAKA 2014 AMBAO WAMECHAGULIWA KUFANYA USAILI KABLA YA KUJIUNGA NA JESHI LA POLISI.

MAJINA YA VIJANA HAO YANAPATIKANA KWENYE TOVUTI YA TAMISEMI www.pmoralg.go.tz AU www.policeforce.go.tzNA OFISI YA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA ILIYOPO FOREST YA ZAMANI KARIBU NA MAHAKAMA KUU.

KWA MKOA WA MBEYA, USAILI UTAFANYIKA TAREHE 09.07.2015 NA TAREHE 10.07.2015 KUANZIA SAA 02:00 ASUBUHI HADI SAA 10:00 JIONI KATIKA SHULE YA SEKONDARI “MBEYA DAY”.

VIJANA WATAKAOFANYIWA USAILI WAFIKE NA:-

1. CHETI HALISI CHA KUZALIWA 2. RESULT SLIP YA KIDATO CHA NNE 3. LEAVING CERTIFICATE YA KIDATO CHA NNE.

IMETOLEWA NA: 
[AHMED Z. MSANGI – SACP] 
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment