Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa wanachama wa chama hicho walioomba ridhaa ya chama kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya Urais iwapo majina yao yatakatwa.
Kauli
hiyo imetolewa mjini Dodoma jana na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa
Chama hicho, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari wakati
akitoa taarifa ya ratiba ya vikao vya mchujo wa wagombea..
Nape
alisema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwasababu, kwanza hakuna
kanuni hiyo na pia hakutakuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo.
“Tuwe
wakweli tu, muda wenyewe siuoni na kanuni haisemi habari ya kukata
rufaa…uchujaji wa majini kikao hakitakiwi kutoa sababu, sasa unakataje
rufaa,” alisema Nape.
Hata
hivyo Nape amewapa matumaini wanachama wa chama hicho kuwa watatoka kwa
umoja hata baada ya kupatikana kwa mgombea urais kupitia chama hicho.
Aidha alibainisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea, kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi vimejipanga vya kutosha.
0 comments :
Post a Comment