Mtaturu akisisitiza jambo wakati wa mkutano
Na Mathias Canal, Mufindi
Wakazi wa
Mtaa wa Kinyanambo, Kata ya Kinyanambo, Wilayani Mufindi wameaswa
kuchagua viongozi watakaowaletea maendeleo katika mitaa yao ili
kukabiliana na mabadiliko ya kujitegemea kwa Mamlaka ya mji wa Mafinga.
Akihutubia
wananchi waliojitokeza Katika Mtaa wa Kinyanambo, mkutano huo wa
kampeni kwa ajili ya viongozi wa serikali za Mitaa, Vitingoji na Vijiji
ambapo uchaguzi unatarajia kufanyika Disemba 14, Katibu wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Mufindi, Miraji Mtaturu, alisema kuwa wananchi
wanapaswa kuchagua viongozi watakaowatumikia kwa ufanisi na uwezo
mkubwa kwa miaka mitano ijayo.
Alisema
kuchagua viongozi wa vyama vya upinzani ni kufunga shughuli za maendeleo
hivyo ni vyema kuchagua CCM ili kuendelea kukamilisha ahadi na ilani ya
chama hicho.
"Ni bora
kuwa mchawi kuliko mnafiki, mimi nawahakikishia kuwa vyama vya upinzani
ni maalumu kwa ajili ya kuvuna pesa za wananchi( SACCOS) sio kwa ajili
ya maendeleo yao" Alisema Mtaturu
Mtaturu
alisema watanzania wanapaswa kutambua kuwa uchaguzi wa serikali za
mitaa, vitongoji na vijiji ni muhimu kwa kuwa viongozi hao ndio
wachapaji kazi za wananchi na wanatekelezaji kazi za wananchi kwa
ufasahasa katika kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
"Kuna
msemo waswahili wanasema usione vyaelea ujue.....wananchi wakaitikia
VIMEUNDWA, basi kama mnalijua hilo msidanganywe na vyama vya msimu
ambavyo havijui kwamba sisi tunatekeleza ilani ya chama na safari hii
tumeianza muda mrefu hivyo abiria anayepandia njiani hawezi kujua nauli
ya mwanzo wa safari" Alisema Mtaturu
Alisema
kuwa Hakuna binadamu anayeweza kumsafisha binadamu mwenzake wakati
mikono yake ni michafu, hivyo vyama vya upinzani vimekuwa vikiikosoa
sana serikali kwa kila jambo inalolifanya pasipo kujali kuwa ni baya au
zuri wakati vyama hivyo havina jambo lolote la kujivunia kwa maendeleo
ya watanzania zaidi ya maandamano na vurugu ambazo zimesababisha
wananchi wengi kupata ulemavu na wengine kupoteza maisha.
Mtaturu
alitumia nafasi hiyo pia kuwanadi wagombea wote wanaowania nafasi za
uongozi katika Mitaa mbalimbali ambapo wananchi walionekana kuitikia kwa
wingi kufurahia wagombea wanaowania nafasi hizo jambo ambalo CCM imeona
kuwa linaendelea kujenga imani ya chama hicho kwa wakazi wa Kinyanambo
na Taifa kwa ujumla.
Alisema
CCM ina amini katika misingi ya uvumilivu, heshima na nidhamu ndio maana
hata wabunge wake huchangia hoja mbalimbali bungeni pasipo jazba na
hasira badala yake hutumia hekima na ustaarabu wakiamini kwamba wananchi
wanawasikia kwa kila jambo wanalolifanya.
Aidha
alisema kuwa CCM ni chama kisichochagua wananchi wa kuwatumikia bali
huwapa nafasi wananchi wake kuchagua viongozi wao wanaowataka katika
ngazi mbalimbali kwani kufanya hivyo ni kutenganisha uongo na ukweli
ambao wananchi wengi wanahitaji kufahamu.
0 comments :
Post a Comment