-->

MTANZANIA AHUKUMIWA KWENDA JELA MAISHA NCHINI AUSTRALIA

http://resources1.news.com.au/images/2014/12/18/1227160/528269-888e2566-8655-11e4-bf87-d1f7005bd55e.jpg 
Charles Mihayo akipelekwa gerezani baada ya hukumu yake. 

MTANZANIA Charles Mihayo (36), ambaye amechukua uraia wa Australia, amehukumiwa kifungo cha maisha jela, baada ya kupatikana na hatia ya kuua watoto wake wawili wa kike Aprili mwaka huu. 

Watoto waliouawa ni Savannah (4) na Indianna (3), ambao Mihayo aliwaua kwa kuwaziba pumzi kwa mto wa kulalia. Vifo vya watoto hao vimeacha simanzi kwani kwa mujibu wa Mihayo, alifanya ukatili huo kutokana na chuki aliyonayo dhidi ya mama wa watoto hao, ambaye ameshatengana naye kwa muda sasa.

Katika uchunguzi wa mauaji hayo yaliyotokea Aprili 20, mwaka huu huko Melbourne, Australia, Mihayo aliwaambia Polisi ilikuwa ni lazima afanye hivyo.

Siku ya mauaji Uchunguzi umeonesha kuwa siku moja kabla ya mauaji, Mihayo alimtumia ujumbe mfupi wa simu mzazi mwenzie akimuomba aone watoto wake kwa mara ya mwisho, na kumwambia kuwa ameshinda. 
http://www.bongo5.com/wp-content/uploads/2014/12/watoto-wa-mihayo.jpgKatika maandalizi ya kuona watoto hao, ambao walikuwa wapelekwe nyumbani kwa baba yao, Mihayo aliwanunualia nguo mpya na viatu na kisha walipofika kumuona baba yao, aliwavalisha na kucheza nao. Wakati akicheza na malaika hao, Mihayo aliyekuwa akicheza na watoto wake, aliamua kuwaua kwa kuwanyima pumzi kwa kutumia mto wa kulalia.

Baada ya mauaji Baada ya kufanikisha unyama huo, Mihayo aliogesha miili ya watoto wake kisha akaivalisha nguo zao, ndipo akapiga simu Polisi kutoa taarifa.

Hata hivyo, baada ya muda mama wa watoto hao aliyekuwa nje ya nyumba hiyo akisubiri watoto wamalize kucheza na baba yao, aliona kimya na ndipo akaenda kwenye mlango wa mzazi mwenzake na kugonga na kujibiwa asubiri kidogo ataona.

Wakati huo Polisi walifika na kugonga mlango na kisha Mihayo akafungua mlango huku akisema ‘nimeshamaliza, nimewaua, nimeua watoto wangu’. Sababu, adhabu Polisi waliofika waliuliza kwa nini ameua watoto wake na Mihayo alimuangalia mzazi mwenzie na kusema “muulizeni huyu”.

Ila mwishowe aliwaambia askari Polisi:”Hamtaelewa nini kinanisibu kufanya haya, na hata nikitoa sababu haitasaidia,” alisema Mihayo. Baada ya mauaji hayo, familia ya mwanamama huyo ilitoa tamko ikisema “hakuna adhabu ya kutosha au kifungo kinachoweza kuondoa huzuni zetu kuhusu tukio hili, tutawakumbuka, na tuliwapenda sana hatutasahau”.

“Tunawashukuru wote wanaoendelea kutufariji kwa sala na maombi katika kipindi chote kigumu, tunatoa shukrani zetu kwa Polisi na maafisa washauri waliotusaidia,” lilisomeka tamko hilo.

Akisoma hukumu hiyo juzi, Jaji wa Mahakama Kuu ya Victoria mjini Melbourne, Lex Lasry, alisema ukatili uliofanywa na Mihayo ni tukio moja baya ambalo anapaswa kupewa adhabu ya kutumikia miaka 40 jela, na kisha kutumikia kifungo cha maisha.

Alisema ni lazima vyombo vya haki vijifunze kupitia tukio hilo na kubainisha wazazi wenye roho za kikatili kama hiyo ya Mihayo, ili kutoa ulinzi kwa watoto na kuepuka madhara kama hayo yasitokee tena.HABARILEO
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment