Huwezi
kuepuka matangazo ya mauzo kila utembeapo katika Mji wa Seoul,utapata
wito wa kukutaka ubadilishe umbo kwa njia ya upasuaji wa kuongeza urembo
bandia.Katika mtaa wa ukwasi wa Gangnam,kila ukuta una ishara ya kukuelekeza sehemu ya upasuaji wa aina hiiKwenye
treni na mitaani,unaelezewa kuwa ''unaweza kurudisha uchanga usoni
mwako.''kuweka ama kuondoa mikunjo usoni'' inapendekezwa
kufanyiwa-''upasuaji wa matiti'',''kuzuia kuzeeka'' ''kubadili kope za
macho''''kupunguza nyama na ngozi inayolegea mwilini''.
Pia kuna
''kupunguza taya na kuzifanya mraba''(matangazo haya hasa huashiria
wanaume).Ama kubadili uso wako ''kutoka ngozi ilioangika na isiyo imara
hadi ile inayojivuta na bora.'' ambayo inaelekezwa kwa wanawake.
Rafiki
yangu mmoja analalamika kuwa huwa anahisi uchungu kwenye kidevu kila
kunaponyesha.Imeibuka kuwa alienda kufanyiwa upasuaji wa pua na
akashawishiwa -ama akajishawishi- kuwa ni mikunjo ya kidevu chake
iliyohitaji kubadilishwa.
Matokeo,kidevu
chenye umbo bora zaidi lakini chenye uchungu zaidi.Licha ya
hayo,anadhamiria kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti.
'Uasi mkubwa'
Katika
nchi hii,wazazi wananielezea kuwa wanawapa mabinti zao zawadi ya
'upasuaji maradufu wa vibugiko vya macho'' inayowezesha macho yao
kuonekana zaidi-''kwa kweli huku ni kupunguza maumbile ya Kiaasia.Sijui
mbona kwani macho ya Kikorea yanavutia sana vile yalivyo.
''Msisitizo
unaotolewa na matangazo ya aina hii kwenye treni ni kuwa ''kujiamini
jinsi unayoonekana hukupa nguvu ambayo yaweza kuwa chanzo cha
furaha.''Furaha ambayo inayopatikana kwa kukatwa kwa kisu!!!
Isipokuwa
kwamba si hivyo.sasa kuna kesi kadhaa kotini ambapo wagonjwa-ama
waathirika kama wanavyojulikana- wanawashitaki madaktari waliopangua na
kupanga tena nyuso zao,kwa njia wasizopenda wao.Muathiriwa mmja alisema
''hii si sura ya binadamu'' punde alipovua bandeji.
Hii si sura ya binadamu,ni maasi kuliko wa hayawani ama majitu.''
'Gharama si mchezo'
Kim
Bok-soon alitumia Won milioni 30 (£17,320) kwa jumla ya upasuaji mara 15
kwenye uso wake katika kipindi cha siku moja na baadaye akagundua kuwa
daktari wake hakuwa mpasuaji wa kuongeza urembo bandia mwilini ambaye
alimhadaa Kim BoK-Soon kutumia won (17,320) kufanya upasuaji mara 15
kwenye uso wake.
Sehemu ya
shida ni kuwa upasuaji wa kuongeza urembo bandia una faida kubwa na kwa
hivyo unawaalika madaktari wengi ambao hawajahitimu- ama madaktari wale
waliohitimu katika nyanya zingine za utabibu.
Inadaiwa
kuwa taratibu zimefanywa na wanaoitwa ''madaktari mapepo''.Katika kesi
moja kotini,inadaiwa kuwa daktari alihepa chumba cha upasuaji wakati
mgonjwa wake akiwa kwenye dawa za kuondoa fahamu na kupunguza uchungu na
kuwacha kazi hiyo kufanywa na mpasuaji mwingine badala yake.
Juu ya
hiyo, iliibuka kuwa madakatari hao wamejifanyia upasuaji wa kujiongeza
urembo bandia kuilingana na picha zao kabla - na - baada ya upasuaji.
Kwa
uhakika ni kwamba Chama cha madaktari wa upasuaji wa kuongeza urembo
bandia Korea kimetoa wito kwa kuwepo na sheria kali ya madaktari na
wanaotoa ujumbe. Wanahofia kwamba utangazaji mbaya unaharibu sifa ya
sekta ambayo kwa kiasi kikubwa imesimamiwa vizuri.
'Biashara kubwa'
Lakini
wao wanapigana na mseto huu, Upasuaji una faida sana, hata una bei
ambazo zinadhoofisha upasuaji huo Marekani na Ulaya. Ni biashara kubwa
sana huko Gangnam, hapa katika Seoul, bei ya "kurekebisha jicho" ni dola
1500 na ni shughuli inayochukua dakka 30 tu. hiyo huongezeka hadi dola
11,000 kwa upasuaji wa kurekebisha sura.
Lakini
labda watu wa China ambao wanataka kuwa kwenye filamu au, wazazi wa
Korea Kusini ambao wanadhani wanaweza kuwarembesha mabinti wao kupitia
kisu cha upasuaji lazima watafakari njia ya kushtua ya kupitia kwenye
mahakama.
Malkia
aliyekuwa mshindi wa taji la urembo, alifanyiwa upasuaji wa kukuza kifua
ambayo ilikuwa na madhara makubwa mno kwani upasuaji huo ulifanya titi
lake moja kuwa kubwa kuliko lingine.
Analaumu
madaktari kwa kushindwa na matibabu na pia kwa kutomweleza kwa uwazi ".
Angalia, huna haja ya upasuaji huu" "Upasuaji wa plastiki ni kama madawa
ya kulevya," alisema. "Kukishafanya macho, utataka pua."
Na
madaktari pia hawakwambii kuwa "uko mrembo sana ulivyo bila upasuaji"
Masaibu yanayokupata baadaye kutokana na madhara ya upasuaji huo huwa ni
juu yako mwenyewe.
0 comments :
Post a Comment