Wapiganaji
wa IS wakibeba mabaki ya ndege waliodai kuidungua huko SyriaWapiganaji
wa kundi la Islamic State wamesema kuwa waliidungua ndege ya jeshi la
muungano ,lakini Marekani inasema kuwa ushahidi uliopo unaonyesha kuwa
hilo si kweli.
Jordan ni
miongoni mwa mataifa manne ya kiarabu yaliopo katika muungano wa
majeshi yanayoungwa mkono na Marekani ambayo yameanzisha mashambulizi
dhidi ya wanamgambo wa IS.
Ndege
hiyo aina ya F-16 ni ndege ya kwanza ya jeshi hilo la muungano kupotea
katika maeneo yanayodhibitiwa na IS tangu mashambulizi yaanze mnamo
mwezi Septemba.
Rubani wa ndege iliodaiwa kudunguliwa na wapiganaji wa IS akamatwaPicha za IS zinamuonyesha rubani wa ndege hiyo akikamatwa.
Wamemtaja rubani huyo kuwa Moaz Youssef al-Kasasbeh.
Wakati
huohuo Jordan imesema kuwa hasara iliyopata ya kupoteza ndege yake moja
ya kivita, katika anga linalodhibitiwa na waasi wa Islamic State,
haitayumbisha majeshi yake kuendelea kukabiliana na matendo ya kigaidi.
CHANZO:BBC
0 comments :
Post a Comment