Unapenda Selfie?
Vingi vimesikika, wapo waliokamatwa kwa
sababu walipiga selfie maeneo ambayo hawaruhusiwi kufanya hivyo, hawa
jamaa nao wamejikuta wakipoteza kibarua baada ya kukiuka maadili ya kazi
yao kwakujipiga selfie.
Ni madaktari na manesi, walikuwa chumba
cha operation Hospitali ya Shaanxi, China wakiwa wanaendelea na jukumu
lao basi ikatokea wazo la kupiga selfie, wakati mgonjwa akiwa hana
fahamu kalazwa akisubiri kufanyiwa upasuaji.
Kitendo cha kushare picha hizo kwenye mitandao ya kijamii kilipelekea
madaktari na manesi kadhaa kfukuzwa kazi, huku wengine watatu
wakikabiliana na adhabu ya kukatwa mshahara wa miezi mitatu kila mmoja.
Uongozi wa Hospitali hiyo umeomba radhi
kwa kitendo hicho, huku ukisema kuwa wafanyakazi hao walichukua picha
hiyo kama kumbukumbu ya siku yao ya mwisho kuwa kwenye chumba hicho
kabla hakijafungwa kwa ajili ya kufanyiwa matengenezo.
Nakuhakikishia
kwamba nitakufikishia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari
kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga
na mimi kwa kubonyeza >>>twitter NA Facebook
0 comments :
Post a Comment