-->

NAMNA VYAKULA VYA NGANO JINSI VINAVYOHARIBU AFYA ZETU


Ndugu msomaji wa makala zangu za afya leo pia ninakuletea makala ambayo ukisoma na kuielewa nitakuwa nime okoa wewe na kizazi chako chote. Hivyo ungana nami dr mkumbo katika elimu zinazohusu magonjwa tabia.
Kumekuwa na ongezeko kubwa sana la magonjwa kama uzito kupita kiasi,kisukari,cancer,uvimbe kwenye kizazi yote haya chanzo chake ni kuongezeka kwa utaalamu katika vyakula vyetu vya asili ambavyo babu zetu walitumia.
Leo ningependa kuongelea sana vyakula vifuatavyo ambavyo ni vihatarishi vikubwa vya afya zetu.


1. Vyakula vya ngano
2. Vyakula vyenye sukari nyingi
3. Vyakula vyenye nyuzi nyuzi kidogo


UTANGULIZI
Tafiti zinaonesha kuwa vyakula tunavyo kula kama vyakula vya ngano ambavyo vina kiambata mahususi kiitacho GLUTEN. Hii ni protini ipatikanayo kwenye ngano ina gundi ambayo hushikilia chakula kwa pamoja. Pia vyakula kama vyenye sukari nyingi na nyuzi nyuzi kidogo nazo ni chanzo kikubwa cha matatizo sugu kama kisukari,uzito mkubwa na mengineyo.
SABABU
Utafiti unaonesha kuwa vyakula hivi huharibu ukuta wa umeng'enyaji chakula kutokana na allergy ya hivyo vyakula. Kuta hizo za utumbo mwembamba huvimba na kusababisha vyakula ambavyo avijameng'enywa vizuri kuingia katika mzunguko wa damu na hatimaye kinga ya mwili huanza kupambana na hicho na hatimaye kusababisha kusambaa kwa allergy mwili mzima na kuathiri utendaji kazi wa insulini(insulin resistance). Insulin ni kichocheo kinachosawazisha sukari mwilini.


Kuathiriwa kwa utendaji kazi wa hiki kichocheo..kinarundikana mwilini na kusababisha matatizo makuu haya:
~Insulin huongeza uhifadhi wa mafuta mwilini na haya mafuta huhifadhiwa kwenye sehem za kuhifadhi mafuta.
Ndio maana tafiti zinasema kuwa watu wengi wenye uzito kupita kiasi ukiwapima utakuta kuna kiwango kingi cha insulin kwenye damu lakini sukari ipo kawaida watu kama hawa tunawaita PRE-DIABETES. Asilimia kubwa ya watu tupo katika hili kundi bali hatufanyi uvhunguzi. Hicho ni kiashiria awali cha ugonjwa wa kisukari.
~Kiwango kingi cha insulin kinafanya mtu azeeke mapema hivyo basi ni dhahiri kuwa watu wengi wenye kisukari hudhoofika na kuzeeka kwa kasi.
MIFANO YA TAFITI ZA KISAYANSI
~Utafiti uliofanyika dec,2007 ambao ulihusisha makundi makuu mawili. Kundi la kwanza ni kundi la watu wenye uzito mkubwa kupita kiasi na kundi la pili ni watu wenye uzito wa kawaida.

~~Utafiti huu ulizingatia kuangalia viashiria vya allergy vitokanavyo na vyakula tunavyokula kama mikate na vyakula vyenye sukari nyingi~~
1. C-reactive protein
~hiki ni kiashiria kuwa kuna mpambano unaendelea na umesababisha allergy kwenye njia ya chakula
2. Kuziba kwa mishipa mikubwa ya damu eg Mshipa upelekao damu kichwani CATOTID ARTERY kwa kutumia ultrosound
3. Kipimo cha damu kuangalia kiashiria cha allergy ambayo huchelewa kujitokeza baada ya muda kidogo mwezi hadi week ukiwa umekula vyakula hivi. Hiki kipimo kinaangalia kichocheo kiitwacho IgG.
MATOKEO
~Watu wenye uzito kupita kiasi walionesha kuwa na kiasi kingi cha kiashiria namba moja C-reactive protein mara tatu ya watu wenye uzito wa kawaida.
~Pia wenye uzito mkubwa walionesha kiwango kingi cha IgG
~Watu wenye uzito mkubwa walionesha kwa kutumia ultrasound kuwa na mafuta mengi kwenye mishipa mikubwa ya moyo na inayopeleka damu kichwani.
UTAFITI HUU LIFANYIKA KWA KUTUMIA VITU VIFUATAVYO
~Vyakula vya viwandani
~Antibiotics
~steroids
~Dawa za kuondoa allergy
~Vyakula vya sukari nyingi
~Vyakula vyenye fiber kidogo
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment