Sheikh Shariff Matongo akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)kuhusu ndoto yake ambayo ameoteshwa kuelekea mwaka 2015.
NA CHALILA KIBUDA,GLOBU YA JAMII,DAR.
Sheikh Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015 na kupata ushauri kwa mashekh mbalimbali duniani ambavyo vitatokea nchini na viongozi wasipuuze ndoto hiyo. Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba likiwemo la kupata Rais ajaye ambaye kiongozi ambaye muda mwingi ameishi nje ya nchi kwa kufanya kazi.
Alisema katika ndoto nyingine kifo cha kiongozi mkubwa ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali na na mwenye kambi katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Sheikh alisema ndoto nyingine kutokea kwa mvua nyingi ambapo watu wanaoishi mabondeni ,kutokea kwa vifo vya watoto vingi ,wafanyabiashara kupata mafanikio makubwa kwa mwaka utaoanza
kesho.
kesho.
Vijana wengi watashinda katika uchaguzi ujao na wazee wataangushwa sana ihivyo wanatakiwa kujitokeza,katiba inayopendekezwa itapita lakini kutakuwa na vurugu ambazo zitaibuliwa na vijana.
‘’Ndoto yangu niliopoteshwa sikukaanyo peke yangu niliweza kupata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Mufti wa wa Abuu Dhabi,Mufti wa Nigeria na wengine wote wanakaniambia suala hilo
nisikaaye nalo nishirikishe na watanzania wenzangu’’alisema Sheikh Shariff
Matongo.
nisikaaye nalo nishirikishe na watanzania wenzangu’’alisema Sheikh Shariff
Matongo.
Sheikh Shariff alisema katika usafiri wa bahari utakuwa mbaya kutokana na bahari kuchafuka na chombo kimoja kitazama kutokana na kuchafuka huko.
Alisema ndoto hizo ni lazima kuweza kuzingatia kutokana na kupata ushauri wa watu wengi wenye kuaminika katika jamii katika mataifa mbalimbali ulimwenguni.
0 comments :
Post a Comment