Askofu mkuu mstaafu wa Cape
Town, Desmond Tutu, ameahirisha mipango ya ziara zake kwa mwaka mzima ujao
kutokana na sababu za kiafya.
Taarifa iliyotolewa na taasisi yake imeeleza kuwa Askofu huyo ataanza matibabu hivi karibuni ili kukabiliana na tezi dume ambayo amedumu nayo miaka kumi na mitano iliyopita.
Binti wa Askofu huyo amemuelezea baba yake mwenye umri wa miaka 82, kwamba hatahudhuria tuzo za Nobel zitakazo fanyika baadaye wiki hii huko Rome, Italia.BBC
0 comments :
Post a Comment