Anaye
daiwa kuwa Daktari feki ,akiwa chini ya ulinzi Dar es Salaam jana, baada
ya kuingia katika Taasisi ya Mifupa (MOI) akiwa amvalia nguo ya kazi na
akiwa na kitambulisho cha kazi na kujifanya yeye ni Daktari wa Taasisi
hiyo .Baada ya kukamatwa na askari alikutwa na vitu mbalimbali kama
vile nyaraka za Serekali,(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Daktari feki aitwaye Dismas Macha amekamatwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI) akiwa
amevaa sare za kazi kama Daktari ambapo hii inakuwa mara ya pili
kukamatwa akiwa anachangisha rambirambi kwa Madaktari akidai kuwa
amefiwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu na Upasuaji wa Ubongo ya MOI, Dk Othman Wanin Kiloloma amesema; “Tumekuwa
tuna tatizo kubwa la kuletewa watu wanaokuja wao na kujitia ni
madaktari wakiomba watu pesa, wakiomba waweze kupewa takrima na hata
michango mingine na wamefikia hatua sasa ya kuwatapeli hata madaktari
wenyewe kwa kuomba michango na vitu vingine“
0 comments :
Post a Comment