-->

ZANZIBAR, HIZI NI SIASA ZA CHUKI AU NI MAANDALIZI YA “MAGOLI YA MKONO”?

ZANZIBAR, HIZI NI SIASA ZA CHUKI AU NI MAANDALIZI YA “MAGOLI LA MKONO”?
Picha hizi ni za mwananchi wa Zanzibar, ambaye nimeambiwa ni mfuasi wa CUF, amepigwa risasi leo na watu wanaodhaniwa kuwa ni JANJAWEED (waliokuwa wamejifunika nyuso) na wanatembea na MASHINE GUN kweupee!
Mtu huyu inasadikiwa amepigwa risasi maeneo ya MAKUNDUCHI (Zanzibar) akiwa kwenye harakati za kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura.
Miezi michache iliyopita wanachama wa CUF walipigwa na nondo na vifaa vyenye ncha kali na kuumizwa vibaya, mmoja alifanyiwa upasuaji mkubwa na iliwapasa madaktari wafumue sehemu yote ya uso hadi mdomoni ili kumuokoa.
Siasa za chuki na uhasama zimeanza Zanzibar na mimi naamini kuwa huwenda CCM imezidiwa mno kwenye uchaguzi wa mwaka huu visiwani humo, na njia pekee ni kuanza kutisha wafuasi wa vyama ambavyo vinaweza kuiondoa CCM mwaka huu.
Najiuliza, je tunahitaji machafuko, vita na uhasama kwa sababu ya madaraka? Je, hatuko tayari kabisa kuacha haki za kidemokrasia za wananchi zitendeke na wajipatie viongozi wanaowataka? Najiuliza yale maridhiano ya mwaka 2010 ya UTANGAMANO wa Zanzibar yako wapi?
Najiuliza, haya ndiyo maandalizi ya "MABAO YA MKONO" ya ndugu yangu Nape?
J. Mtatiro,
DSM.
 
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment