E, UNAJUA WATANZANIA ZAIDI YA MILIONI 20 HAWANA AJIRA RASMI?
Hadi tarehe ya leo kuna zaidi ya Watanzania milioni 23 kwenye soko la ajira ambao hawajaajiriwa. Kila mwaka kuna ongezeko la vijana zaidi ya laki tisa kwenye soko la ajira, ndiyo kusema kuwa baada ya miaka mitano ijayo, kutakuwa na vijana milioni tano wameongezeka kwenye soko la ajira na tutakuwa na jumla ya takribani nguvu kazi ya watu milioni 30 wasio na ajira.
Ndiyo maana nchi yetu inahitaji mfumo mpya na uongozi mpya wa kisiasa kupambana na tatizo la ajira, ndiyo maana ukweli uko wazi kwamba CCM imeshindwa kabisa kutatua changamoto ya ajira kwa vijana.

Taifa hili
linahitaji uongozi mpya, utakaokuja na mfumo mpya wa kushughulikia kila
jambo, uongozi utakaokuja na majibu tofauti kwa maswali ambayo yamekuwa
na majibu yale yale kila siku "...mchakato unaendelea....tutahakikisha
tumelishughulikia...liko mbioni kukamilika....lilikwama kwa sababu ya
ukosefu wa fedha.....tutaliangalia...tutalifuatilia...."
J. Mtatiro
DSM.
J. Mtatiro
DSM.
0 comments :
Post a Comment