Vyombo vingi vinamshambulia Messi kwa kusema kwamba kukataa kupokea tuzo ya mchezaji bora wa Copa America ni ambacho sio cha kimichezo. Kuna video inaonyesha jinsi official mmoja wa Copa America akiitoa tuzo hiyo ya mchezaji bora kwenye steji ya kupokea medali.
Messi alipita hapo bila kuchukua hiyo tuzo. Lakini taarifa nyingine mpya zinasema kwamba Messi hakukataa kupokea tuzo hiyo bali ameichukua. Alichokiomba ni kwamba hataka kupewa pale kwenye steji ya kushangilia. Lakini alimwambia mmoja ya afisa wa Copa America kwamba tuzo yake apewe nje ya steji ile ndio maana hakuipokea pale na alipelekewa baadae kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Tusubili taarifa zaidi kuhusu hii habari lakini kwa sasa hii ndio habari kamili. Hii ndio video ikionyesha afisa wa Copa America akiitoa tuzo hiyo kwenye steji.
0 comments :
Post a Comment