Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa hafla fupi ya
Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano ya kuhifadhi
Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama, iliyofanyika
kwenye Msikiti wa Istiqaam, Ilala jijini Dar es Salaam jana usiku.
(Picha na OMR).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi Cheki ya Sh. Milioni 3, mshindi wa kwanza wa Mashindano ya
Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu, Said Nassor Said, aliyehifadhi Juzuu
30, wakati wa hafla fupi ya Utoaji wa Tuzo na Kuwakirimu washindi hao wa
mashindano yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama. Hafla hiyo
ilifanyika kwenye Msikiti wa Istiqaama Ilala jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na Balozi wa Iran nchini Tanzania, Mehdi Aghajafari, wakati
akiondoka kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki
swala ya Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano
ya Tano ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya
Istiqaama.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal,
akiagana na baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu wakati akiondoka
kwenye Msikiti wa Istiqaama jana usiku baada ya kushiriki swala ya
Talaweh na kukabidhi Tuzo za Kuwakirimu washindi wa Mashindano ya Tano
ya kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyoandaliwa na Taasisi ya Istiqaama.
(Picha na OMR).
0 comments :
Post a Comment