-->

JULIUS MTATIRO AMCHAMBUA LOWASA KINAGA UBAGA BAADA YA KUCHEMKA URAIS CCM


NILIANDIKA HAYA KUHUSU EDWARD LOWASSA MIEZI MIWILI ILIYOPITA, MNAKUMBUKA?
1. (Nguvu ya Lowassa ndani ya CCM haimithiliki na hofu ya chama hicho kuwa kumuacha nje ya ulingo kutakitetemesha haikwepeki. Lakini ukweli naouona ni kuwa ndani ya CCM “kuna minofu mingi” sana ambayo inawazuia vigogo wakubwa wasiondoke na kuhamia vyama vingine hata kama hawakupitishwa kugombea urais. “There is too much stake to eat in CCM than getting out”. )
2. (Ndiyo maana bado CCM ina nafasi ya kujichagulia mgombea inayemtaka, na vigogo wanaotajwa kuitikisa kama Lowassa wakiogopa kuondoka kwa sababu wamekaa serikalini muda mrefu na sasa hawawezi kumalizia maisha bila mfumo huo waliouzoea.)
3. (Kwa hiyo, nadhani Lowassa ataendelea kuwa mwanachama mtiifu kwa CCM akiwa Rais na au akiwa Raia wa kawaida. Na kama kuna vyama vya upinzani vilikuwa “vinamtumbulia” macho kama fisi asubirivyo mkono wa binadamu udondoke, ni vema vijipange kupata wagombea wake imara na vijijenge.......)
J. Mtatiro
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment