Askari kanzu akikagua mwili wa mwanafunzi huyo leo
barua yenye ujumbe aliouacha marehemu huyo.
--------
Mwanafunzi aliyekuwa akisoma
shule ya sekondari Sabasaba mjini Iringa akijiandaa kurudia
kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne kupitia kituo cha
Krelluu mjini Iringa Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata C katika
manispaa ya Iringa amejiua kwa kujinyonga kwa kamba kwa kile
alichodai kuchoshwa na kufeli mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.
Katika barua yake ndefu
aliyoiandika kijana huyo amesema kuwa amefanya hivyo si kwa
kujipendea ila amechukizwa na hatua yake ya kufeli mara kwa mara
hiyo kuamua kujiua ili kuepuka na aibu katika mtihani ujao ambao
anaamini angefeli.
Shemeji wa kijana huyo Aden Tagalile
ameueleza mtandao huu kuwa tukio hilo
limetokea muda wa kati ya saa 12 na saa 1 usiku wa jana baada ya
kuwepo kwa mazungumzo ya muda mrefu kwa kijana huyo kuonyesha
kuchukia hatua yake ya kuendelea 'kurisiti' mtihani wa kidato cha nne
bila mafanikio.
Kwani alisema hajapenda kuona anaendelea kufeli na kuwa yupo tayari kwa lolote kukwepa aibu ambayo ipo mbele yake.
Hata hivyo kufuatia mazungumzo hayo
kijana huyo aliangana na ndugu zake akiwemo kaka yake anayeishi naye kwa
kila mmoja kuondoka nyumbani hapo kabla ya kijana huyo kukutwa
amejinyonga.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo
Sarehe Mgimwa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuonyesha ujumbe
ambao kijana huyo ameuacha.
Kuona habari hii na picha nyingi za tukio hilo tafadhali bonyeza link hiyo hapo mbele ya chanzo cha habari hii www.matukiodaima.com
0 comments :
Post a Comment