Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa
Pensheni wa PPF, William Erio akimuongoza Sheikh wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa Salum na wadau wa mfuko huo kupakua futari
iliyoandaliwa na PPF Kanda ya Temeke kwa wadau wake, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF, William Erio akizungumza na wadau wa mfuko huo baada
ya kupata futari iliyoandaliwa na PPF Kanda ya Temeke, Dar es Salaam.
Wengine kutoka kulia kwake) ni Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad
Mussa Salum, Mwakilishi wa Sheikh wa Wilaya ya Temeke, Sadi Msati na
Msaidizi wa Sheikh Ahad Musa, Athumani Mkambaku.
Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, akitoa shukrani zake baada ya futari hiyo.
Sheikh Alhadi, akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa PPF, Erio.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF, William Erio akimkabidhi Sheikh wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Alhad Mussa Salum zawadi iliyotolewa na mfuko huo Kanda ya
Temeke kwake baada ya kupata futari iliyoandaliwa na PPF Kanda ya
Temeke, Dar es Salaam.
Wadau wa Mfuko wa Pensheni
wa PPF na wafanyakazi wa Mfuko huo, wakipakua futari iliyoandaliwa na
PPF Kanda ya Temeke kwao, Dar es Salaam.
0 comments :
Post a Comment