Winga wa Manchester United Luis
Nani Jumapili atatua Instanbul kwa ajili ya kukamilisha vipimo vya afya
kwa ajili ya kujiunga na klabu ya Fenerbahce ya Uturuki.
Taarifa kutoka Fenerbahce
imethibitisha: “Fenerbahce imefungua majadiliano na Luis Nani na klabu
yake ya Manchester United kwa ajili ya kumsajili mchezaji huyo”.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa
Ureno, alisaini mkataba wa miaka mitano mwaka 2013 kuitumkia United
wakati David Moyes alipokuwa kocha wa Manchester.
Lakini baada ya kocha huyo
kutimuliwa, nafai ya Nani ilikuwa ndogo kwenye kikosi cha Old Trafford
hasa pale alipotua kocha mpya Louis van Gaal ambaye alionekana hana
mipango ya baadae na Nani.
0 comments :
Post a Comment