Dalili za mwanzoni ni kichefuchefu, mara nyingine kutapika, maumivu sehemu ya katikati ya tumbo, homa na kutetemeka, kutopata haja.
Ni takriban wiki mbili zilizopita mmoja wa wanahabari wetu wa Mwananchi alinusurika katika hatari ya kufa baada ya kupatwa na tatizo hili la kidole tumbo.
Hili lilimtokea ghafla akiwa mkoani Dodoma kwa
ajili ya majukumu yake ya kawaida ya kikazi na kulazimika kufanyiwa
upasujai wa dharura.
Ni mengi yameulizwa baada ya tukio hilo.
Tunaposema kidole tumbo au kwa lugha ya kitaalamu appendix, tunamaanisha
ni sehemu ya utumbo iliyo na umbile kama kidole na uwazi kama kijibomba
inayoning’inia katika makutano ya utumbo mpana na mdogo katika sehemu
ya upande wa kulia wa tumbo.
Mpaka dakika hii wanasayansi hawajui kijinyama
hiki kina kazi gani, ingawa wapo wanasayansi waliowahi kusema kuwa
yalikuwa ni makosa ya kiuumbaji na kwamba haikupaswa kuwepo katika
tumbo.
Katika nchi zilizoendelea, wao huamua kuwafanyia
upasuaji watoto wao wanapozaliwa kwa kuondolewa mapema ili kuepuka
kadhia hii pale ukubwani, pia tatizo hili halijulikani ni kwa nini
linawapata baadhi ya watu tu.
Tatizo hili haliwapati watoto wenye umri chini ya
miaka miwili na huwapata zaidi watu wenye umri kati ya 15-30, huku
wanaume ndiyo wanaongoza kwa kupata ugonjwa huu. Inaonyesha kuwa watoto
wanne kati ya 1,000 walio katika umri wa miaka 14 hupatwa na ugonjwa huu
na kulazimika kufanyiwa upasuaji.
Dalili za uambukizi wa kidole tumbo
Ilikuwaa ni saa nne asubuhi pale nilipoanza
kujisikia maumivu upande wa kulia chini ya tumbo, yalikuwa ya ghafla na
taratibu huku yakiongezeka na kuwa makali yasiyovumilika, mwanahabari
wetu anaeleza.
Hata hivyo, kwa jumla dalili si lazima zijitokeze
zote, lakini dalili za mwanzo zinazojitokeza ni kichefuchefu, mara
nyingine kutapika, kuumia upande wachini wa kulia wa tumbo pale
unapominya, maumivi sehemu ya katikati ya tumbo na unapominya sehemu
hiyo maumivu huweza kusambaa na kusikia maumivu upande wa chini wa
kulia, maumivu hayo huweza kuongezeka pale unaposogea, kukohoa au kupiga
chafya.
Dalili nyingine ni kama vile homa na kutetemeka,
kutokupata haja, kushindwa kuhimili kupitisha gesi ya tumboni kwa njia
ya haja kubwa, tumbo kuvimba, kuharisha na kukosa hamu ya kula.
Basi kwa dalili hizo hapo pale unapoona dalili ni vyema kufika katika huduma za afya mapema.
CHANZO:MWANANCHI
CHANZO:MWANANCHI
0 comments :
Post a Comment