WACHEZAJI Soka huko England na Scotland wamealikwa kuisaidia Kampeni ya kuunga mkonoMashoga kwa kutakiwa kufunga Nyuzi za Rangi ya ‘Upinde wa Mvua’ kwenye Buti zai wakati wa Mechi za Wikiendi hii inayokuja.
Tayari Taasisi ya Hisani ya Mashoga,
Stonewall, imetuma Nyuzi hizo spesho kwa Vilabu 92 vya Ligi Kuu England
na Klabu za Ligi za Madaraja ya chini na pia Klabu 42 za Soka ya Kulipwa
huko Scotland.
Kwenye Kampeni hii, iitwayo The Right
Behind Gay Footballers, Wachezaji wataombwa kutumia Nyuzi hizo kwenye
Mechi za Septemba 21 na 22.
+++++++++++++++++++++++
KLABU 29 ZINAZOSAPOTI MASHOGA:
-LIGI KUU ENGLAND: Arsenal, Aston Villa, Crystal Palace, Liverpool, Manchester City, Norwich, Sunderland, West Ham, West Brom
-CHAMPIONSHIP: Birmingham, Blackburn, Doncaster, Huddersfield, Ipswich, Leicester, Millwall, Sheffield Wednesday
-LIGI 1: Carlisle, Crewe, Gillingham, Leyton Orient, MK Dons, Peterborough, Preston, Tranmere
-LIGI 2: Bristol Rovers, Exeter, Dagenham & Redbridge, Northampton
**LISTI IMEHAKIKIWA TAREHE 18 Machi 2013
+++++++++++++++++++++++
Huko Uingereza, haki za Mashoga zinalindwa na hata FA ina msimamo wa kukemea Mashoga kubaguliwa.
Kwa sasa hakuna hata Mchezaji mmoja huko Uingereza alieibuka bayana na kukiri yeye ni Shoga.
Mwaka 1990, Mchezaji wa zamani wa Timu
ya Taifa ya England ya U-21 pamoja, Justin Fashanu, alikuwa ni Mchezaji
wa kwanza wa Kulipwa kutangaza yeye ni Shoga lakini Mwaka 1998, Fashanu
alijiua mwenyewe akiwa na Miaka 37.
SOURCE:SOKA IN BONGO
0 comments :
Post a Comment