Mark youssef Basseley mtengeneza filamu
ya ‘The Innocence of Muslims’ inayomkashifu Mtume Muhammad SAW na
iliyosababisha maandamano makubwa duniani na kupelekea vifo vya watu
kadhaa pamoja na balozi wa Marekani nchini Libya, ameachiliwa huru
alhamisi amethibitisha mwanasheria wake.
Basseley alikuwa anatumikia kifungo cha mwaka mmoja kwa kukiuka masharti ya hukumu iliyotolewa 2010 ya kosa la udanganyifu. Alikuwa akitumikia adhabu hiyo katika kituo cha magereza huko Taxes.
Basseley aliwahi kutupwa jela miaka mitatu iliyopita kutokana na utapeli wa cheki za watu kwa kutumia majina mbalimbali feki. Alikaa jela mwaka mmoja kabla ya kutolewa kwa masharti kumalizia kifungo chake uraiani.Kujihusisha kwake kutengeneza filamu hiyo, kumevunja masharti aliyopewa hivyo akarudishwa jela kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela.
Kwa sasa atakuwa chini ya usimamizi kwa muda wa miaka minne kuangalia mwenendo wake katika jamii, kwa kutorudia makosa aliyotenda au kuiumiza jamii kwa namna yoyote ile. Hata hivyo haijaeleweka wapi ataishi na itakuwaje. Basseley amekuwa akiwindwa vikali na jamii ya kiislamu kwa ajili ya kuadabishwa kwa kile alichokitenda cha kuukashifu Uislamu na Mtume Muhammad SAW.
Basseley, ambaye ni tapeli mwenye kujipa majina mbalimbali mwenye umri wa miaka 56 aliwahi kuhukumiwa kwenda jela miezi 21 nchini Marekani kwa makosa mbalimbali ya utapeli, aliingia mafichoni pamoja na familia yake baada ya maandamano ya kuipinga filamu aliyoitengenza kuzidi kupamba moto.
Basseley alijiita jina la Sam Bacile wakati wa utengenezaji wa filamu ya "The Innocence of Muslims" ambayo trela lake lenye dakina 14 liliwekwa kwenye YouTube na video zake zikimuonyesha mtu aliyeigiza kama Mtume Muhammad, akifanya mapenzi, akibaka na akiamuru kuuliwa kwa watu.
Basseley au Nakoula Basseley Nakoula, hajaonekana hadharani tangu kuitoa filamu hiyo, polisi walimsaidia kumficha kwa kwenda nyumbani kwake kuichukua familia yake ya watu wanne, kisha kumhamisha kwenda mafichoni kusikojulikana. Polisi wa Los Angeles waliwasili majira ya alfajiri kabla jua halijachomoza na walimchukua mke wa Basseley na watoto wake watatu na kuwasindikiza kwenye maficho ya siri ambako Nakoula alikuwa amejificha.

Familia yake ilizificha sura zao wakati
wakisindikwa na polisi toka kwenye nyumba yao iliyozungukwa na waandishi
wa habari wengi waliokuwa wakikesha mbele ya nyumba hiyo.
"Tulichokifanya sisi ni kuwachukua na kuwapeleka sehemu ambayo Basseley amejificha", alisema msemaji wa polisi.

Baadae mahakama iliamuru akamatwe kwa
kosa la kuvunja masharti ya hukumu aliyopewa ya kosa la utapeli. Katika
mahojiano aliyowahi kufanya na CNN Basseley alisema, “kamwe sikufikiria filamu yangu ingeweza kusababisha maumivu kwa watu au kufa kwa sababu ya filamu yangu.”
Anasema alitengeneza filamu hiyo ili
kuweka wazi ukweli halisi kuhusu Mtume Muhammad SAW katika unyanyasaji
wake kwa kivuli cha ishara ya Mwenyezi Mungu.
0 comments :
Post a Comment