-->

WANAFUNZI WAKIKE WATAABIKA NCHINI INDIA,NA KULAZIMIKA KUOMBA MAKOTI ILI WAJINUSURU NA MAFATAKI PAMOJA NA WABAKAJI


Chama cha upinzani cha India, BJP, kimeiomba serikali ya mji wa Pondicherry, kusini mwa nchi, kuwapatia watoto wa shule makoti wavae ili wasinyanyaswe kijinsia.
Katibu wa chama alitoa taarifa kusema kuwa unyanyasaji ni tatizo hasa katika shule za serikali, na kwamba wasichana wote wapewe makoti na piya wapate fursa ya kueleza malalamiko yao bila ya kujitambulisha.
Visa vya ubakaji vimezidi kuripotiwa nchini India na kupelekea sheria mpya kupitishwa.
Lakini baadhi ya viongozi wamelaumiwa kwa kutazama maisha ya wanawake tu, badala ya kubadilisha tabia za wanaume.
Maandamano dhidi ya ubakaji India
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment