Dar es Salaam/Nairobi.
RAIA wa Nigeria aliyefukuzwa Kenya miezi minne iliyopita kwa kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya, amekamatwa tena nchini humo akiwa na pakiti 425 za heroin, akiamin
ika kwamba alipitia Tanzania.
RAIA wa Nigeria aliyefukuzwa Kenya miezi minne iliyopita kwa kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya, amekamatwa tena nchini humo akiwa na pakiti 425 za heroin, akiamin
ika kwamba alipitia Tanzania.
Mtu huyo aliyetajwa kwa jina la Enobemhe Emmanuel
Peter inaaminika alishukia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Dar es Salaam, akitokea Nigeria na kisha kwenda Kenya kwa
barabara, kupitia mpaka wa Namanga mkoani Arusha.
Peter alikamatwa pamoja na mwanamke ambaye ni raia
wa Kenya, usiku wa Ijumaa iliyopita jijini Nairobi na anatarajiwa
kufikishwa mahakamani leo.
Raia huyo wa Nigeria ni kati ya wageni
waliofukuzwa nchini humo Juni mwaka huu kwa agizo la Rais wa Kenya,
Uhuru Kenyatta aliyeamuru raia wa kigeni wanaojihusisha na biashara ya
dawa za kulevya wafukuzwe nchini humo.
Mkuu wa Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya
cha Kenya, Dk Hamisi Massa alisema uchunguzi zaidi wa dawa hizo
utafanyika kabla mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani.
“Ni kati ya watu waliokuwa wamefukuzwa nchini
katika nyumba aliyokamatiwa kulikutwa pia na pakiti 425 za heroin,”
alisema Dk Massa.
Mtu huyo amekamatwa kutokana na kuwapo kwa taarifa
zilizoonyesha kuwa, watu wengi waliofukuzwa Kenya kutokana na
kujihusisha na biashara hiyo sasa wamerejea tena.
Julai 9 mwaka huu, Ofisa Uhamiaji wa nchi hiyo,
Edward Kabiu Njau alifikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kumruhusu
Anaeke Chimenze, aliyefukuzwa nchini humo, kurejea tena.
Chimenze ambaye ni raia wa Nigeria mwenye pasi ya
kusafiria namba 02743350, pia anadaiwa kurudi nchini humo kupitia mpaka
wa Namanga.
Uhamiaji Tanzania
Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, Naibu Kamishna,
Abbas Irovya alisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa yupo nje ya
ofisi. “Mtafute Tatu ndiye mtu wa habari zaidi, kama atakuwa amepata
hizo taarifa atakueleza,” alisema.
Mwananchi ilipomtafuta Tatu Iddi alisema hajapata
taarifa hizo na kutaka mwandishi amtumie barua pepe ikiwa na maelezo ya
mtu huyo aliyekamatwa ili aweze kutafuta taarifa zaidi. MWANANCHI
0 comments :
Post a Comment