Umoja wa Falme za Kiarabu, Imarati umemwita nyumbani balozi wake wa
nchini Tunisia kulalamikia wito wa Rais wa nchi hiyo Moncef Marzouki
kutaka Muhammad Morsi, rais wa Misri aliyeondolewa madarakani na jeshi
na kuwekwa kizuizini hadi sasa, aachiliwe huru. Akihutubia mkutano wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa juzi Alkhamisi, Rais wa Tunisia aliwataka
watawala wapya wa Misri wanaoungwa mkono na baadhi ya nchi za Kiarabu
ikiwemo Imarati wamwachie huru Rais halali wa nchi hiyo Muhammad Morsi
aliyeondolewa madarakani Julai 3 katika mapinduzi yaliyoongozwa na
jeshi. Gazeti la Al- Khaleej linaloakisi misimamo ya serikali ya Umoja
wa Falme za Kiarabu limekosoa hotuba ya Rais wa Tunisia kwa kuishambulia
serikali ya mpito ya Misri na kusisitiza kuwa kinachotakiwa kufanywa ni
kuiunga mkono serikali ya Cairo ambayo imekuja madarakani kwa matakwa
ya wananchi. Baada ya jeshi kumuondoa madarakani Morsi, Umoja wa Falme
za Kiarabu, Saudi Arabia na Kuwait ziliunga mkono mapinduzi hayo na
kuahidi kuipatia kwa pamoja Misri msaada wa dola milioni 12 kusaidia
uchumi wake uliozorota…/
source Iran swahili radio
source Iran swahili radio
0 comments :
Post a Comment