Wabunge wa bunge la waakilishi Nigeria wamerushiana ngumi wakati wa
vikao vya Jumanne baada ya kuzuka bungeni suitofahamu kuhusu mrengo wa
wabunge waliojitenga na chama tawala. Taarifa hizi ni kwa mujibu wa
vyombo vya habari nchini humo.
Chama tawala cha PDP kimekuwa kikikumbwa na mgogoro wa ndani kwa muda sasa
Kituo kimoja cha kibinafsi cha televisheni, pamoja na vituo vingine
vilionyesha picha za mbunge mwanamke akimtosa kidole usoni kwa ghadhabu
mbunge mwenzake wakati mbunge mwanamume akionekana akichukua kiti nusura
kumgonga mwenzake.
Wabunge wengine walionekana wakipigana ngumi.
Mgogoro inasemekana ulianza baada ya mwenyekiti
wa mrengo wa wabunge waliojiondoa kutoka kwa chama tawala, Kawu Baraje,
kuingia bungeni akiandamana na magavana wanaomuunga mkono.
Inaarifiwa spika wa bunge la waakilishi ,Aminu
Tambuwal, aliambia wabunge kuwa Baraje aliomba ruhusa kuwahutubia
wabunge wa mrengo wake kabla ya bunge kuanza vikao vyake.
Lakini kuwepo kwa wabunge hao bungeni
kuliwaghabisha mno wafuasi wa chama tawala, PDP,kiasi cha kuzuka
sokomoko bungeni kati ya pande hizo mbili na kumlazimisha bwana Baraje
kukatiza hotuba yake kutokana na kelele bungeni.
Chama tawala PDP kina wabunge wengi zaidi bungeni wakiwa 23 kati ya wabunge wote 36
Aidha chama hicho kimetawala Nigeria tangu
kupata uhuru mwaka 1999 lakini hivi kribuni kimezongwa na migogoro ya
ndani ya chama pamoja na kukabiliwa na upizani wenye ushawishi.
Wananchi wanajiandaa kwa uchaguzi mwaka 2015,
lakini wadadisi wana wasiwai ikiwa chama tawala kitakuwa kimesuluhisha
migogoro yake, huku kikikabiliwa na upinzani mkali.
Mgogoro huu umekuwa ukitokota kwa miezi kadhaa
huku baadhi ya wabunge wakitofautiana kuhusu ikiwa Rais Goodluck
Jonathan aidhinishwe na chama kugombea urais kwa mara nyingine wakati
kuna wanasiasa wengine wanaotaka kugombea urais.
Hii ni mara ya kwanza kwa wabunge wa Nigeria kurushiana ngumi bungeni
0 comments :
Post a Comment