HABARI KUTOKA AHBAABUR RASUUL
Wimbo wa mwanamuziki wa POP wa kimarekani Stefani Joanne
Angelina Germanotta 27, maarufu kama Lady Gaga umezua mtafaruku na kuwasha hasira za waislamu baada ya
kuonekana unadhalilisha mavazi ya wanawake wa kiislam.Wimbo huo mpya ulioutambulishwa
hivi karibuni unajulikana kwa jina la Burqa.
Burqa (برقع) ni vazi linalovaliwa na wanawake wa kiislam wakiwa katika mkusanyiko wa
watu.Vazi hili ni maarufu sana kwa wanawake wa Afghanistan na ulaya.Na sasa
limepata umaarufu sehemu malimbali duniani.Vazi la stara ni sheria kwa mwanamke
wa kiislamu kwa mujibu wa Qurani Tukufu
Kutokana na hilo watu wamepinga wimbo huo wa msanii Lady Gaga kutokana na
yale maisha anayoishi msanii huyo.Kwamba
maudhui ya wimbo yanaonekana yanadhalilisha wanawake wa kiislam kwa
maneno yaliyomo katika wimbo wa msanii huyo.
Baadhi ya maneno yaliyokuwemo ndani ya wimbo huo yanasema
" I'm not a
wandering slave, I am a woman of choice
My veil is protection for the gorgeousness of my face, Do you wanna see me naked, lover?
Do you wanna peek underneath the cover? Enigma popstar is fun, she wear
burqa for fashion
It's not a statement as much as just a move of passion”
Kwa tafsiri isiyo rasmi ni kwamba, "mimi si mtumwa ninayegaagaa, ni mwanamke
mwenye kujielewa.
Hijabu yangu ni kinga ya urembo wa sura yangu,unataka kuniona nikiwa
mtupu,mpenzi?
Unataka kufikia kilicho chini ya stara? Enigma nyota wa pop anachekesha. Anavaa
hijabu kama fasheni,Siyo kufikisha ujumbe bali kutimiza matakwa yake”
Mwanamuziki huyo mwenye kupendelea kukaa wazi sehemu kubwa ya mwili wake,amejiwa
juu na wanawake wa kiislamu kwa udhalilishaji wa vazi hilo tukufu.Aidha
mwenyewe lady Gaga anasema amefanya hivyo ili kulitia nguvu vazi hilo kwa
jamii.Hata hivyo amepingwa vikali na wanawake wa kiislamu wa nchini Pakistani
kwa kuambiwa vazi hilo haliitaji kutangazwa kwani ni amri iliyotoka kwa
mwenyezi Mungu kwa mwanamke wa kiislamu kuvaa kwa kustiri maungo yake.
Kwa kuthibitisha hilo walinukuu aya isemayo “Na waambie waislamu wanawake
wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao wala wasidhihirishe viungo vyao,isipokuwa
vinavyodhihirika( uso na vitanga vya mikono). Na waangushe shungi zao mpaka
vifuani mwao,na wasioneshe mapambo yao ila kwa waume zao,au baba zao,au baba za
waume (wakwe zao) au watoto wao,au wanawake wenzao………..” Aya hiyo ipo katika Surat Nnur aya ya 31
Mwanamuziki huyo bado hajatoa video ya wimbo huo,ila amejitokeza hadharani
akiwa amevaa vazi hilo huku akiachia wazi sehemu ya maungo yake.Vita dhidi ya
uislamu imekuwa ikifanywa na watu mbalimbali duniani ambapo matokeo yake
yamefanya watu wengi kuingia katika uislamu kinyume na matarajio ya wanaoupiga
vita. Baadhi ya nchi za ulaya wamekuwa wakilipiga vita vazi hilo la Burqa
Lady Gaga |
Lady Gaga |
Mwanamke wa kiislamu |
wanawake wa kiislamu |
0 comments :
Post a Comment