-->

KITU KINCHOSADIKIKA KUWA BOMU CHATUPWA ZANZIBAR DARAJANI



Picture
Msaidizi wa Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar, Mkadam Khamis Mkadam
Washambuliaji wasiojulikana walitupa guruneti karibu na eneo la biashara kando ya Barabara ya Darajani huko Zanzibar mapema Jumatatu asubuhi (tarehe 23 Septemba), viongozi wa usalama waliiambia Sabahi.
 Msaidizi wa Kamishna wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar Mkadam Khamis Mkadam alisema mlinzi binafsi, Amour Kassim Amour, mwenye miaka 36, ambaye alikuwa kazini Duka la Sahara, aliona idadi ya watu katika gari aina ya 'pickup' wakija kuelekea dukani alipokuwa akilinda wakati mmoja wao aliporusha guruneti upande wake.
"[Guruneti] lilikuwa likitoa moshi. Kwa ushujaa, Amour aliliokota na kulitupa mbali na maduka," Mkadam aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba guruneti lililipuka kwa mlipuko wenye sauti kubwa dakika chache baadaye. "Kwa bahati, Amour alilitupa kwenye uwanja wa wazi na hakukuwa na wanunuzi katika mtaa huo wenye shughuli nyingi kwa sababu ilikuwa ni usiku."
Polisi wameanzisha msako na uchunguzi katika tukio hilo, Mkadam alisema, akiwataka Wazanzibari kuwa watulivu na kuripoti kitu chochote kinachoshukiwa.
SABAHOLINE
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment