Said Salim Awadh Bakhresa.
KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri alionekana ni hatari
kwa taifa, tena mali zake alizimiliki kwa kificho, vinginevyo angeitwa
mhujumu uchumi. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za
kibepari zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.
Mtu kama ni mbunifu, ana
nidhamu ya kutofuja pesa na anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri?
Utandawazi unasaidia ndiyo maana leo tunaweza kuwatambua mabilionea
wakubwa ambao wanastahili pongezi kwa hatua walizopiga. Tusisahau kuwa
wanaibeba nchi kwa ulipaji kodi.
1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa.
Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40
Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620
(karibu shilingi trilioni moja). Hata hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya
usiri wa Bakhresa inafanya mali zake zisijulikane sana, ila ni tajiri
zaidi ya kiwango hicho.
Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa
yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali
Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa
majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika. Ndiye
mmiliki wa Klabu ya Azam FC.
2. GULAM DEWJI
Huyu ni baba wa mfanyabiashara maarufu nchini,
Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa na
utajiri wenye thamani ya dola milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900).
Mafanikio yake kibiashara yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st
Century Textiles, kinatajwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo
Afrika.
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani ya dola
milioni 420 (shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia 40 ya hisa
Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian
inayohusika na uchimbaji wa madini na ukandarasi nchini Tanzania, nchi
kadhaa za Afrika na Asia.
4. DK. REGINALD MENGI
Anatajwa kumiliki utajiri wenye thamani ya
dola milioni 280 (karibu shilingi bilioni 450). Ni mmiliki wa kundi la
makampuni ya IPP, yanayomiliki vyombo vya habari, viwanda, migodi ya
dhahabu, Tanzanite na kadhalika.
5. ALI MUFURUKI
Utajiri wake unatajwa kuwa na thamani ya dola
milioni 110 (shilingi bilioni 176). Ni mmiliki wa kundi la makumpuni ya
Infortech Investment, inayomiliki maduka yanayouza vitu vya rejareja
Tanzania na Uganda. Vilevile ana vitega uchumi vingine.
6. MUSTAFA SABODO
Ni mfayabiashara mkubwa sana nchini anayemwaga
mamilioni kwa misaada. Wakati wa kuanzishwa kwake, aliipa Taasisi ya
Mwalimu Nyerere shilingi milioni 800, akasaidia shilingi milioni 100
katika mradi wa kustawisha mimea jamii ya kunde. Vilevile alikipa
Chadema shilingi milioni 300. Inadaiwa kuwa utajiri wake unazidi
shilingi bilioni 100. Kampuni yake ya Khoja Shia Itnasheri Jamat (KSIJ),
ndiyo yeye tenda ya kujenga maeneo ya maegesho ya magari Posta, Dar es
Salaam, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 5.6.
7. ABDUL-AZIZ ABOOD
Kiwango chake cha utajiri hakiwekwi sana wazi
lakini anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 10 wanaotikisa nchi kwa
sasa. Anamiliki viwanda kadhaa mkoani Morogoro, vyombo vya habari, Abood
Radio na TV. Anamiliki mabasi ambayo yanafanya safari zake kati ya
Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam. Ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM).
8. MICHAEL SHIRIMA
Ni mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege la
Precision ambalo linafaya safari zake ndani ya Tanzania pamoja na nchi
mbalimbali za Afrika. Ana asilimia tano ya hisa katika Beki ya I&M
(Tanzania), vilevile ni memba katika bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo
yenye thamani ta shilingi bilioni 200. Hisa zake Precision ni asilimia
42.91.
9. YUSUF MANJI
Kiwango halisi cha utajiri wake bado hakifahamiki
lakini anafahamika kama mmoja wa mabilionea wakubwa nchini Tanzania. Ni
mmiliki wa makampuni ya Quality Group na majengo ya Quality Centre,
Quality Plaza na kadhalika. Ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na utajiri
wake umeifaya timu kutotetereka tangu alipoanza kuiongoza.
10. MOHAMMED DEWJI
Baba yake anashika nafasi ya pili katika orodha
hii. Dewji au Mo kama anavyoitwa na wengi, anatajwa kuwa bilionea
nambari moja katika orodha ya mabilionea vijana Afrika (orodha hiyo
tuliitoa wiki iliyopita). Ni mmiliki wa makampuni ya Mohammed
Enterprises Tanzania Limited (METL) ambayo inatengeneza faida ya
shilingi bilioni 136 kwa mwaka
CLICK HAPA CHINI ILI KUIPIGIA KURA www.goohlehabari.blogspot.com kuwa BLOG BORA
WEBLOG AWARDS 2014
hivi mtu unaweza ukawa katika top 100 ya matajiri kwa kublog? hebu wanablog niambieni muonavyo
ReplyDelete