Maofisa wakiingia eneo la wahamiaji haramu kutekeleza
oparesheni Kimbunga
|
Maofisa wakiingia eneo la wahamiaji haramu kutekeleza
oparesheni Kimbunga
|
Maofisa wakiingia eneo la wahamiaji haramu kutekeleza
oparesheni Kimbunga
|
Wahamiaji wakiwa katika kambi ya kuwakusanyia mjini Bukoba |
Wahamiaji wakinywa chai kusubiri kuondolewa nchini katika kambi ya kuwakusanyia iliyopo Kagemu nje kidogo ya mji wa Bukoba |
Oparesheni Kimbunga imeendelea kutimua vumbi katika mkoa wa
Kagera ambapo wahamiaji mamia wameshakamatwa na kuanza kurudishwa makwao. Hadi sasa
jumla ya wahamiaji 400 wamesharudishwa katika nchi za Rwanda, Burundi na
Uganda.
Mmoja wa askari anayeshiriki katika oparesheni hiyo
alimweleza bloga wetu kuwa idadi kubwa ya raia wa Rwanda wamekataa kurudi kwao
na kudai kuwa wao ni raia wa Tanzania hali iliyowafanya maofisa wanaowapokea
wahamiaji hao katika mpaka wa Rusumo upande wa Rwanda kukataa kuwapokea.
‘’Kuna baadhi ya wahamiaji karibu 70 wamekana kwamba wao sio
raia wa Rwanda nah ivy maofisa wa Rwanda walikataa kuwapoke.’’ Alisema mtonyaji
wetu huyo.
Zoezi la kuwatimua wahamiaji haramu katika mikoa ya Geita,
Kigoma na Kagera lilioanza siku 10 zilizopita ni utekelezaji wa agizo la raia
kuwaondoa wale wote wanaoishi nchini kiunyume cha sheria za uhamiaji.
0 comments :
Post a Comment