Mwandishi Jamal Osman amefanya mahojiano exclusive na msemaji wa kundi la kigaidi la Al-Shabaab kuhusiana na sababu za kuishambulia mall ya Westgate.
Hii ni tafsiri ya Kiswahili ya mahojiano hayo yaliyofanywa kwa Kiingereza kwenye mtandao wa Channel4
Jamal Osman: Kwanini mmefanya shambulio?
Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu
ya kufanya shambulio ni kuwalinda watu wetu na nchi yetu sababu Kenya
ilitushambulia, bado wanaendelea kushikilia sehemu ya ardhi yetu.
Tumekuwa majirani wenye amani, lakini wao ndio walitushambulia na
tunajilinda.
Haijalishi kama wewe ni Muislamu ama Mkristo, sheria inasema unatakiwa kujilinda mwenyewe dhidi ya yule aliyekushambulia.
JO: Mmeua watu wa mataifa mengi wakiwemo Waingereza, hamuogopi mataifa makubwa yatawatafuta?
Msemaji wa Al-Shabaab: Tumewaambia
Wakenya na wale wanaoenda Kenya kwamba hatuwezi kuvumilia kile Kenya
inatufanyia. Tuliwaambia tutajilinda wenyewe na tuliwaonya kuhusu kwenda
Kenya.
Wakenya
wana damu yetu mikononi mwao. Mtu yeyote aliyejiandaa kwenda Kenya
lazima ajiandae na kukabiliana na ukweli huo, na hatuwaogopi watu wa
Ulaya ama Wamarekani sababu sisi si wadhaifu.
Na
tunasema hili kwa watu wa Ulaya na Wamarekani ambao wamekuwa
wakiwasaidia wale wanaotushambulia, muwaambie Wakenya waache uonevu wao
kama mnataka kuwa salama.
JO: Kwanini mliilenga mall ya Westgate?
Msemaji wa Al-Shabaab: Sababu
ya kwanini tuliilenga mall ya Westgate, ni kwakuwa Wakenya na serikali
yao wametumia majeshi dhidi yetu, ni maadui wetu. Wamewatuma watu wao
Somalia, wameiunga mkono serikali yao kuishambulia nchi yetu. Kwetu,
popote pale Kenya ni sawa, tutawapiga popote tuwezapo.
Sababu
tulilenga Westgate ni kwamba tunajua ni sehemu ambayo wanajisikia
maumivu zaidi. Ni kwasababu inaingiza hela nyingi na ipo katikati ya
jiji.
Ni
sehemu wanasikia maumivu na kwasababu tulitaka kutuma ujumbe na
hatukutaka kuupoteza ujumbe wetu. Tulitaka ujumbe wetu umfikia kile
Mkenya.
JO: Wapiganaji wenu ndani ya mall bado wanapigana?
Msemaji: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
Msemaji: Ni zaidi ya saa 27 sasa, wapo ndani na bado wameshika hatamu.
JO: Nasikia kuna mpiganaji mwanamke ndani pia?
Msemaji: Hatupeleki wanawake wetu kwenye uwanja wa vita.
JO: Kitu gani mnategemea kitatokea sasa? Nini litakuwa tokeo la hili?
Msemaji: Kama
Mungu akipenda, tunategemea Wakenya watapata ujumbe kwamba kama
ukimwaga damu, damu yako itamwagika pia. Kwao kujua kuwa hawawezi
kushikilia Kismayu, Dhobley na Afmadow na wategemee waishi kwa amani
Nairobi. Huo ni ujumbe tunataka kuutuma kwao.
JO. Kwenye jumbe zenu kupitia Twitter mnasema huu ni mwanzo tu na mtaendelea, ama mmeshafikia malengo yenu?
Msemaji: Tunasema
kwa Kenya, iacheni nchi yetu. Huo ni ujumbe wa kwanza. Na kama
wakikataa kuiacha nchi yetu basi tutaanzisha vita yenyewe.
JO: Hivyo matakwa yenu kwa Wakenya, ni kuiacha nchi yenu kama wanataka amani?
Msemaji: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
Msemaji: Kama Wakenya wanataka amani, wanatakiwa kuiacha nchi yetu.
JO: Kwanini mnawalenga watu wasio na hatia?
Msemaji: Raia
wa kigeni, wanatakiwa kuondoka kwenye nchi hiyo (Kenya) kwasababu
Wakenya na Al-Shabaab wapo kwenye mgogoro na tunamwambia kila mtu –
Kenya ni eneo la vita.
JO: Kwakuwa unasema raia wa kigeni na Waingereza wana maslahi makubwa nchini Kenya, mna ujumbe gani kwao?
Msemaji: Tunasema kwa Waingereza, kwakuwa tunaamini wanawasaidia Wakenyan na Wakenya ni watumwa wao, wao (Waingereza) wanatakiwa kuwaambia Wakenya, walitoe jeshi lao Somalia.
Na Waingereza wanajua Wasomali hawataka tamaa. Tuliwakatalia Waingereza mwanzoni, ambao wana nguvu kuliko Wakenya
SOURCE:MUSLIM OF AFRICA
0 comments :
Post a Comment