Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema itafungua mashtaka dhidi ya kampuni ya Gold Star, baada ya meli yake kukamatwa na tani 30 Za mihadarati aina ya bangi Kisiwa cha Malta Vessel, nchini Italia.
Hatua hiyo ilitangazwa na Mkurugenzi wa Mamalaka ya Usafiri Baharini (ZMA), Abdi Omar Maalim, alipozungumza ofisini kwake Mlandege Zanzibar, jana.
Maalim
alisema kwa mujbu wa sheria namba 5 ya mwaka 2006 ya usafiri baharini,
kampuni hiyo imekiuka masharti ya usajili, ambayo yanazuia meli kubeba
silaha, dawa za kulevya, wakimbizi au mzigo wowote wenye biashara
haramu.
Alisema
wanasheria wa ZMA wataipitia sheria hiyo kabla ya kuamua kuishtaki
kampuni hiyo mabaharia tisa wanaodaiwa kula njma za kusafirisha bangi,
kabla ya kukamatwa huko Italia.
“Tunategemea
kufungua mashtaka dhidi ya Kampuni ya Gold Star kwa kukiuka masharti ya
fomu ya usajili, ambayo yanazuia meli kubeba mihadarati, silaha,
wakimbizi au mzigo wowote haramu,” alisema Maalim.
Alisema
meli hiyo ilisajiliwa Oktoba 5, 2011 na Kampuni ya Uwakala wa Kusajili
Meli ya Philtex Corparation yenye kituo chake kikubwa cha biashara
nchini Dubai, inamilikiwa na raia wa Marekani na Phillipines.
Maalim alisema Kampuni ya Philtex ina mkataba wa miaka 10 wa kusajili meli na SMZ, ikiwa na hisa asilimia 35 na SMZ 65.
Alisema
mkataba huo ulitiwa saini mwaka 2007 na umeweka sharti kuwa, hakuna
kampuni yoyote yenye mamlaka ya kusajili meli kwa niaba ya SMZ zaidi ya
kampuni hiyo hadi miaka 10 itakapoisha.
Alisema
kulingana na mkataba huo, upande wowote utakaovunja masharti kabla ya
muda kumalizika utalazimika kulipa fidia ya dola 500,000 za Marekani na
kusisitiza kuwa, Philtex haina makosa kufuatia meli hiyo kukamatwa na bangi kwa vile ni uhalifu wa kawaida kama inavyotokea kwa meli nyingine.“Iran imewekewa vikwazo na Baraza la Usalama wa UN, zilifutiwa usajili wake baada ya kujitokeza malalamiko ya Zanzibar kusajili meli za mafuta za Iran,” alisema
0 comments :
Post a Comment