-->

JOPO LA MAIMAMU KUKUTANA NA PAPA FRANCIS ILI KUIMARISHA MAHUSIANO YA KIDINI

Kundi la maimamu 10 wa kifaransa watakutana na Papa Francis Jumatano ijayo mjini Roma kama ishara ya kutengeneza uhusiano kati ya Vatican na ulimwengu wa Kiislamu.

Mkutano huo Umeandaliwa na Marek Halter, mwandishi wa Kifaransa mwenye asili ya kiyahudi mtu maalumu kwa ajili ya kukuza uvumilivu wa kidini ambapo mikutano kama hiyo amewahi kuandaa siku za nyuma.

“Nafikiri Papa huyu anaweza kufanya kile ambacho Papa aliyepita hakufanya. Yeye anaweza kupatanisha Ukristo na Uislamu,” alisema Halter. Mahusiano kati ya Vatican na ulimwengu wa kiislamu yaliathirika katika miaka ya karibuni wakati chuo kikuu cha kiislamu cha Misri, Azhary walipovunja uhusiano na Papa aliyepita Benedict XVI wakati alipotoa kauli za utata juu ya tukio la mtu kujilipua na bomu katika kanisa moja Misri mwaka 2011.

Papa Francis ameonesha ishara kadhaa za maridhiano ambapo mwezi Agosti  aliuita mwezi wa kuheshimiana baina ya Uislamu na Ukristo.


Hassen Chalghoumi ambaye ni kiongozi wa jumuiya ya kiislamu katika kitongoji cha Paris atakuwa ni miongoni mwa watakaosafiri kwenda mjini Roma kwa ndege ya shirika la Tunisia na madai yake ni kufutwa kwa sharia ya kuzuia Kuvaa vazi la Burqa nchini Ufaransa.

SOURCE:AHBAABUR  
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment