-->

TATIZO LA MAJI NCHINI SWEEDEN LACHUKULIWA KAMA LA MGONJWA MAHUTUTI

Gari hii  inayojulikana uswahilini kama "kimurimuri" hutumika kufuatilia matatizo ya maji yanayotokea katika Manispaliti ya Kiruna nchini Sweden.
Matatizo ya maji yakitokea hushughulikiwa kama mgonjwa mahatuti anayepelekwa hospitali. Taa zinazoonekana juu huwaka kuonyesha ishara gari nyengine zipishe ili mafundi wafike haraka kwenye tatizo la maji.
Shirika letu la maji ZAWA,DAWASCO.MOROWASCO na mengineyo wana mengi ya kujifunza hapa Kiruna Sweden ili huduma zetu za maji ziwe bora.

Aidha wananchi wetu nao wana mengi ya kujifunza kuhusu utunzaji wa vianzio vya maji pamoja na ulipaji wa huduma hiyo kwa wakati.

Picha na Maelezo kutoka kwa Mohamed Muombwa, Kiruna Sweden
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment