-->

URUSI NA UFARANSA WAMTIKISA OBAMA KATIKA SWALA LA SYRIA

Urusi na Ufaransa zimeeleza wazi wazi tofauti zao kuhusu ripoti ya wataalamu wa silaha wa Umoja wa Mataifa, ambayo ilithibitisha kwamba silaha za kemikali zilitumiwa nchini Syria. 
Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Urusi Sergei Lavrov ambaye alikutana na mwenzake wa Ufaransa Laurent Fabius mjini Moscow jana, alitupilia mbali madai kwamba serikali ya Syria ndio iliyotumia silaha hizo katika mashambulizi ya Agosti 21 karibu na Damascus.

Ingawa ripoti hiyo haikusema upande gani ulitumia silaha hizo, Laurent Fabius alisema hakuna shaka lolote kwamba serikali ya rais Bashar al-Assad ndio iliyofanya mashambulizi hayo, ambayo Marekani inasema yaliuwa watu zaidi ya 1400.

Lavrov alisema hakuna ushahidi wowote kuthibitisha madai hayo, na alikariri msimamo wa nchi yake kwamba silaha hizo zilitumiwa na waasi ili kuzivuta nchi za magharibi ziingilie kati kijeshi.
SOURCE:PERUZI BONGO
Share on Google Plus

About Omari Makoo

    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments :

Post a Comment