Wachezaji wawili wenye historia ya kuweka rekodi ya kuwa wachezaji ghali kuliko wote hii leo wamekutana kwa mara ya kwanza kabla ya mazoezi ya timu yao .
Gareth Bale na Cristiano Ronaldo walikutana kwa mara ya kwanza tangu wakati Bale aliposajiliwa na Real Madrid toka klabu ya Tottenham Hotspurs .
Bale amevunja rekodi ya Cristiano Ronaldo baada ya usajili wake kwenda Real Madrid kuigharimu klabu hiyo ya Hispania paundi milioni 86 akiwa ameuzidi usajili wa Ronaldo kwa paundi mdilioni 6.
Bale na Ronaldo walikutana hii leo mapema dakika chache kabla ya kuanza kwa mazoezi ya Real Madrid wakiwa wamejiunga na klabu hiyo baada ya kuziacha kambi za timu zao za taifa .
Bale alicheza kwenye mechi mbili za Wales ikiwemo mechi dhidi ya Macedonia iliyochezwa jana huku Ronaldo akicheza na kuifungia Ureno kwenye mchezo dhidi ya Ireland Ya Kaskazini na aliukosa mchezo wa jana kati ya Ureno na Brazil.
0 comments :
Post a Comment